Home » » KIWANGO CHA MAAMBUKIZI YA UKIMWI CHA SHUKA KWA ASILIMIA 3.5 MKOANI GEITA

KIWANGO CHA MAAMBUKIZI YA UKIMWI CHA SHUKA KWA ASILIMIA 3.5 MKOANI GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiwahutubia wananchi wa Kijiji na Kata ya Nyawilimilwa Wilaya ya Geita wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi  akipanda Mti kwenye moja kati ya maeneo ambapo kuna zahanati ya kijiji cha Nyawilimilwa.

Mkuu wa Wilaya  ya Geita,Mwl Herman Kapufi akipanda mti kwenye zahanati ya Kijiji.

Mratibu wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Ukimwi Mkoa wa Geita,Dkt   Joseph  Odero akimuelezea Mkuu wa Mkoa ,Mhandisi Robert Luhumbi namna zoezi la upimaji linavyoendelea Kijijini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akipewa maelezo na moja kati ya wahudumu wakati alipotembelea banda la huduma za afya kijijini hapo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita,Dkt Japhet Simeo akitoa taarifa ya Mkoa juu ya shughuli ya upimaji na watu ambao wameathirika na virusi vya Ukimwi. 

Baadhi ya viongozi wakimsikiliza mkuu wa Mkoa wakati alipokuwa akihutubia.


Mkuu wa Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa,Mhandisi Robert Luhumbi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akitoa msaada kwa watoto ambao ni yatima waliondokewa na wazazi kutokana na ugonjwa wa UKIMWI.




Na ,Faudhia Sharifu,Geita


Jumla ya watu 1,412 sawa na asilimia 3.5 wameathirika na virusi vya ukimwi Mkoani Geita uku wanawake wakiwa ni 828 na wanaume wakiwa Ni 584.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya  siku ya ukimwi Duniani ambayo kimkoa yemefanyika kwenye kijiji na kata ya Nyawilimilwa, Mganga Mkuu wa Mkoa wa huo Dkt Japhet Simeo amesema Takwimu za upimaji wa virusi vya UKIMWI ngazi ya jamii Jumla ya watu waliopimwa maambukizi ya VVU katika kipindi cha Aprili hadi Septemba 2017 ni 40,910 wanaume wakiwa ni 22,569 na wanawake 18,341 na ambao wamekutwa na maambukizi  ni 1,412.

Na kwamba kutokana na hali hiyo Kiwango kimeendelea kupungua kutokana na mbinu na mikakati mbalimbali za Mkoa dhidi ya maambukizi ya UKIMWI.

Aidha Dkt Simeo  ameongeza kuwa Jumla ya wagonjwa 65,825  ambapo wanaume ni 24,812 na Wanawake  41013 Wamekwishaandikishwa kwenye vituo vya Tiba na matunzo ,ambapo ni  kuanzia 2012 – Septemba, 2017kati ya hao walioanzishwa dawa ni 52,550  wakiwemo wanaume  19296 na wanawake   33,254  na wanaoendelea na dawa (matibabu ni 32,709  wanaume  11188, na  wanawake  19914) ambayo ni sawa na 62.2.

Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho  hayo,Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema kuwa kundi kubwa ambalo linaongoza kwa maambukizi ni vijana  ambao wanakuwa kwenye umri wa miaka 15 hadi 25 huku wanawake na mabinti wakiongoza kwa kiasi kikubwa Mkoani humo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi  kwenye kijiji hicho,Devid Maduka,ameshukuru zoezi la upimaji kuwepo kijijini hapo huku akiomba serikali kutoa walau siku nyingi za upimaji.


Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani   Kitaifa yamefanyika Jijini Dar es salaam huku kauli mbiu ikisema i “Changia mfuko wa udhamini wa ukimwi okoa maisha tanzaniabila ukimwi inawezekana”

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa