Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita akitoa maelekezo kwa Mkuu wa
Wilaya ya Geita(Wakwanza kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Nguzombili wakati wa ziara yake katika Shule hiyo.
|
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiingia ndani ya moja ya darasa lililojenjwa chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya Msingi Nguzo Mbili. |
Vyumba vya madarasa vilivyojengwa kupitia mpango wa lipa kwa matokeo Halmashauri ya Mji Geita. |
|
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Lughumbi ameipongeza Halmashauri ya
Mji wa Geita kwa kusimamia vizuri fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa
vilivyo chini ya mpango wa lipa kwa matokeo shule ya msingi Nguzo
mbili.
Akizungumza
wakati wa ziara yake katika shule hiyo Mheshimiwa Robert Gabriel
alisema kuwa ameridhishwa na kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi
wa madarasa kwa ubora wa hali ya juu katika shule hiyo.
"
Inashangaza sana kuona maeneo mengine wanatumia fedha zote kiasi cha
shilingi 20 milioni katika ujenzi wa darasa moja lakini kuna mapungufu
mengi hivyo lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha katika miradi ya
Serikali"Alisema Lughumbi.
Akiwa
shuleni hapo Mkuu wa Mkoa ameagiza wakurugenzi kuunda na kutumia
vikundi vya ujenzi vilivyo katika maeneo ya utekelezaji wa miradi ya
ujenzi wa madarasa pia kuishirikisha jamii ili kupunguza gharama kwa
serikali na hatimaye fedha zinazobaki ziwezekufanya mambo mengine katika
huduma za jamii.
Katika
hatua nyingine Mhandisi Robert Gabriel aliutaka uongozi wa Shule ya
Msingi Nguzo Mbili kusimamia suala la usafi na kumuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Geita kuhakikisha anasimamia uimarishaji wa
miundombinu hiyo ambayo mingine imeanza kupasuka.
Aidha,
ameagiza shule hiyo kupelekewa miundombinu ya maji ili vyoo
vilivyojengwa vianze kutumika badala ya kufungwa.Pamoja na kutembelea
Shule ya Msingi Nguzo Mbili Mkuu wa Mkoa pia ameitembelea shule ya
Sekondari na kukagua ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa vilivyojengwa
kupitia mpango wa lipa kwa matokeo.
Shule
ya Msingi Nguzo mbili imejenga madarasa nane kwa kutumia shilingi
milioni 13 kwa kila darasa, Ofisi 4, kisima cha maji na vyoo vya kisasa
pamoja na ukarabati wa madarasa mengine katika shule hiyo kutokana na
fedha iliyobaki katika bajeti ya darasa moja.
Mkoa
wa Geita una upungufu wa vyumba vya madarasa 8600 hivyo serikali
imeandaa mpango kabambe wa kutokomeza tatizo hili kwa kushirikiana na
jamii na wadau wote wa Mkoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa.
0 comments:
Post a Comment