Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabalogi Kijiji cha Kifufu ambaye ambaye ametengwa na wananchi kutokana na kugoma kulipa faini ya shilingi laki sita. |
Diwani wa kata ya Bugalama , Luponya Masalu akiwasisitiza wananchi kuishi kwa amani na kusameheana makosa yao ili kuruhusu maendeleo kwenye Kijiji cha Kifufu. |
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Diwani wakati alipokuwa akihutubia hadhara hiyo. |
Wakina Mama wakifuatilia Mkutano huo. |
Meza kuu ikiongozwa na Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa kikao hicho. |
Wananchi wa Kijiji cha Kifufu Kata ya Bugalama Wilayani Geita wameazimia kumtoza faini ya shilingi laki sita Mwenyekiti
wa kitongoji cha Mwabalogi kutokana na kuwepo kwa tabia ya watoto wake
kuingia kwenye makazi ya wanakijiji na kuiba mifugo pamoja na mazao.
Hata
hivyo mwenyekiti huyo Bw Nchemba Kasomeko amesababisha hali ya
sintofahamu kwa wanakijiji baada ya kugoma kuomba msamaha na kukiri
makosa ambayo yamesababishwa na watoto wake mbele ya mkutano wa hadhara
ulioitishwa na diwani wa kata hiyo uliokuwa na lengo la kuleta suluhu
baina yake na wanakijiji kutokana na tuhuma za kuwahifadhi wahalifu
wakiwemo wajukuu zake jambo ambalo limesababisha uvunjifu wa sheria.
Katika
Mkutano huo Bw Nchemba anadaiwa kuwakejeli wananchi pamoja na viongozi
wa kata wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya kata hiyo
baada ya kumtaka alipe faini ya Sh Laki 6 ya kuhifadhi wahalifu baada ya
wajukuu zake kutuhumiwa kwa wizi wa matikiti maji kwenye shamba la
Leonard Martin kwa kuwaita masikini.
“Ndugu
zanguni mimi nashangaa watu kusongamana kila wakati mnanitafuta mimi
tu,nimekuwa kama dume la wizi na nyie viongozi hapa mbele ni wanafiki tu
na kitu cha kukaa ninasumbuliwa nitoe laki sita wakati sio mwizi wizi ni watoto mliwaachia nyie kuwa mmewasamehee leo tena mnataka nitoe mahela mengi wanakijiji nilishawai kufika kwako nikakomba mboga tatizo umasikini wenu unawasumbua au mnataka nitoke humu nijenge Geita”Alifoka kwenye Mkutano huo.
Kutokana
na Majibu ya Nchemba kuwa ya kejeli na kuto kuafiki kulipa faini ya Sh
Laki 6, baadhi ya wananchi wamechukizwa na kauli zake na kuuomba uongozi
wa kijiji na kata kuondoka nae .
“Kweli
Nchemba asijione anavyo sana kuliko wananchi kama kuna faini naomba
atoe hiyo faini sio yeye ajifanye anavyo sana jamani kwani Mungu aliumba
Masikini na matajiri”Alisema Getruda Kachwele.
“Ndugu
mwenyekiti nadhani Muda unakwenda na hili la Nchemba hatutalimaliza
sisi tulikwisha wapatia mtu wenu mnaonaje kama mtamchukua muende nae tu
maana sisi huyu hatuwezi kuendelea kuwa na mtu wa namna hii kijijini
hapa”Alisikika akisema Musa Msafiri.
Kufuatia
madai hayo kwa wananchi Diwani wa kata Hiyo, Luponya Masalu amemtaka Bw
Nchemba kuwaomba radhi wananchi na kuwalipa wananchi pesa ya faini
ambayo anadaiwa lakini amekaidi na kumtaka diwani kumuacha akajifikirie.
Julai
23 Mwaka huu Mkutano Mkuu wa Kijiji hicho uliketi na kuazimia Bw,
Nchemba alipe kiasi hicho cha fedha ambapo alikubali lakini leo
ameyatupilia mbali maamuzi hayo .
0 comments:
Post a Comment