Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Meja Jenerali (Mst) Ezekiel E. Kyunga
Mkoa huu ulianzishwa mwaka 2012
kutoka sehemu ya mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera ukiundwa na
Wilaya tano zenye Halmashuri Sita na majimbo saba (7) ya Uchaguzi. Mkoa
una ukubwa wa eneo la km2 21,879 linalotumika katika shughuli
za Kilimo cha mazao ya (Nanasi, Mahindi, Mpunga, Alizeti, Pamba na
mazao mengine), Uchimbaji wa Madini aina ya Dhahabu katika Mgodi Mkubwa
wa GGM na migodi midogo midogo, Biashara, Ufugaji, na uvuvi hususan
maeneo ya Wilaya za Geita na Chato. Aidha Mkoa huu unasifika kuwa na
hifadhi ya misitu mikubwa ya Kigosi /Moyowosi na kisiwa cha Rubondo
kilicho ndani ya ziwa Victoria, kisiwa hiki kina wanyama adimu kama
Statunga, Sokwe na eneo la mazalia ya samaki aina ya sangara.
Chanzo Tovuti ya Mkoa wa Geita
0 comments:
Post a Comment