Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Meneja
wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino (kulia) akikabidhi madawati
kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita - Manzie Mangochie (kushoto) kwa niaba ya
Shule za Msingi Nyamkumbu na Ukombozi msaada wa madawati 100 yenye
thamani ya shilingi milioni 10 kutoka Benki ya NMB katika hafla fupi
iliyofanyika mjini Geita jana ambapo kila shule imekabidhiwa madawati
50.
Wanafunzi wa Shule za Msingi Nyankumbu wakiwa na nyuso za furaha
baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 50 na Benki ya NMB jana wilayani
Geita. NMB ilisaidia madawati 100 yenye thamani ya Shilingi milioni 10
katika shule mbili za msingi za Nyamkumbu na Ukombozi ambapo kila shule
ilipata madawati 50.
Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino (kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Manzie Mangochie (kushoto)
pamoja na wanafunzi baada ya makabidhiano ya madawati.
Benki ya NMB jana ilikabidhi msaada wa madawati 100 yenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa Shule za Msingi Nyankumbu na Ukombozi zilizopo mkoani Geita ambapo kila shule imekabidhiwa madawati 50.
Msaada huo umekabidhiwa na meneja wa NMB Kanda ya Ziwa - Abraham Augustino ambapo mkuu wa wilaya ya geita alipokea madawati hayo kwa niaba ya shule hizo mbili za msingi.
“Madawati haya tunayoyakabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania tunahakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata,” alisema Augustino.
0 comments:
Post a Comment