Home » » WANANCHI GEITA WAWALALAMIKIA WAHUDUMU NMB

WANANCHI GEITA WAWALALAMIKIA WAHUDUMU NMB

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wananchi Geita wawalalamikia wahudumu NMB
WANANCHI wanaohudumiwa na benki ya NMB mkoani hapa, wamelalamikia huduma mbovu zinazotolewa na wahudumu wa benki hiyo ikiwamo kuwatolea lugha chafu.
Wakizungumza na Tanzania Daima jana kwa sharti la kutotaka kutajwa majina yao, baadhi ya wateja waliokutwa katika benki hiyo, walisema pamoja na huduma kuwa mbaya, wafanyakazi wamekuwa wakichangia wateja kuhama kutokana na lugha zao.
Waliongeza kuwa, watu wanaotoka vijijini hasa walimu wanaochukua mishahara yao katika benki hiyo, wamekuwa hawathaminiwi wakati wa kupewa huduma na kuomba wafanyakazi hao kunyang’anywa simu zao za mikononi ili watoe huduma kwa ufasaha.
“Mimi nimekuja tangu juzi, nimekuja kuchukua mshahara wangu ni mwalimu wa shule ya Sekondari Nyarugusu, lakini tangu nifike ATM ni mbovu hazitoi pesa, tunapanga foleni mpaka unachoka, ukiuliza unatukanwa na wafanyakazi sijui tufanye nini,” alisema mwalimu huyo.
Meneja wa Benki hiyo, Penina Kilanga, alipoulizwa kuhusu madai hayo, alisema watu ni wengi wanaokuja siku za mwisho wa mwezi, hivyo ATM zao zinaelemewa, lakini kuna njia mbadala kama ‘Sim Banking’ lakini wateja wao wamekuwa hawazitumii.
Penina, alifafanua kuwa, kuhusu majibu mabaya kwa wateja hilo hana taarifa nalo na kuahidi kufuatilia, ikiwemo kuwawajibisha watakaobainika kutenda hayo.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa