Home » » MWANAFUNZI WA KIGOGO WA ELIMU ADAIWA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA SABA MIAKA MIWILI MFULULIZO NA KUPEWA MAJIBU.‏

MWANAFUNZI WA KIGOGO WA ELIMU ADAIWA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA SABA MIAKA MIWILI MFULULIZO NA KUPEWA MAJIBU.‏

Na Mwandishi wetu Geita
MWANAFUNZI aliyefanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka jana anadaiwa kufanya tena mtihani huo mwaka huu kwa kutumia jina lilelile katika shule nyingine ya Kawawa kata ya Kakubilo wilayani Geita.

Mwafunzi huyo,Monica Masunga Sayi(15),aliyemaliza darasa la saba mwaka jana shule ya msingi Kakubilo kwa kufanya mtihani wa Taifa,kudaiwa kufanya mara ya pili mtihani wa darasa la saba mwaka huu.

Mwanafunzi huyo ni mtoto wa Mratibu Elimu kata ya Kakubilo,Masunga Sayi alifanya mtihani huo kwa mara ya pili kwa kutumia jina la Monika Silya Masunga.

Monika anadaiwa kufanya mtihani huo kwa Kutumia jina la Monika Silya Masungau kwenye shule hiyo.

Uchunguzi,umebaini kuwa Mwanafunzi huyo alionekana tu siku ya mtihani hali iliyowafanya wanafunzi wenyeji kumshitushwa na ujio wa Mwanafunzi huyo wa kufika na kufanya mtihani.

Monika,alianza darasa la kwanza shule ya msingi Burigi 2007,kabla ya kuhamia shule ya msingi Kakubilo 2011 akiwa darasa la tano na aliandikishwa kwa Na.4548.

Kwaka jana alikuwa miongoni mwa wanafunzi 78 waliofanya mtihani wa Taifa wa darasa la saba,kwa kutumia Na.PS 2404051/062,Hata hivyo baada ya matokeo kutoka hakufaulu kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari.

HUU NI  MWANZO WA KISA HIKI USIKOSE KESHO ITAENDELEA HAPA HAPA....

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa