Home » » WANAFUNZI WALALA CHINI GEITA

WANAFUNZI WALALA CHINI GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MBUNGE wa Busanda mkoani Geita, Lolensia Bukwiba amemwaga machozi baada ya kukuta wanafunzi wa kike zaidi 25 wa shule ya Sekondari Nyakamwaga wakilala chini kwa kukosa vitanda.
Hali hiyo ilijitokeza jana wakati mbunge huyo alipokuwa akikagua miradi ya visima sita vya maji anavyojenga katika Kata ya Nyakamwaga wilayani Geita kwa kushirikiana na wananchi.
Mbunge huyo alipomaliza kukagua miradi hiyo, alitembelea bweni la wasichana wa shule hiyo na kujionea adha wanayoipata watoto hao wanaolala chini na kujikuta akibubujikwa machozi na kuahidi kutoa sh milioni tano kutoka kwenye mfuko wa jimbo na kuwaomba wahisani na wafanyabishara wengine kusaidia shule hiyo.
”Jamani mimi kama mbunge wa jimbo hili, nimeona hali ilivyo mbaya kwa wanafunzi wa kike wanavyoteseka, sina cha kuogea nawaomba wahisani na wafanyabishara tuungane kusaidia jambo hili,” alisema Bukwimba.
Mkuu wa shule hiyo, Meryciana Deusdedit, alisema kuwa shule yake yenye wanafunzi 319 wa kike wakiwa 188 na walimu 18, imekuwa na changamoto nyingi kama kukosa maabara na uzio, jambo ambalo watoto wa kike wamekuwa wakiishi kwa wasiwasi kwa kuogopa kubakwa wakati wa kuoga.
Aliongeza kuwa watoto wengi wa kike wamekuwa wakianza masomo lakini kutokana na shule hiyo kukosa mabweni ya kutosha, wamekuwa hawamalizi kutokana na kurubuniwa na vijana wa mitaani na kuwapa mimba na kuwakimbia huku wakibaki wakihangaika.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa