Home » » JUST IN: JESHI LA POLISI MKOANI GEITA LAKAMATA BUNDUKI SABA ZILIZOPORWA KITUO CHA POLISI BUKOMBE, MTU MMOJA ATIWA MBARONI

JUST IN: JESHI LA POLISI MKOANI GEITA LAKAMATA BUNDUKI SABA ZILIZOPORWA KITUO CHA POLISI BUKOMBE, MTU MMOJA ATIWA MBARONI



 Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Jeshi la polisi mkoani  Geita limekamata bunduki saba (pichani) na mabomu kadhaa ya machozi eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe ikisadikiwa kuwa ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu  jana. Bunduki hizo, nne zikiwa SMG na tatu aina ya Shotgun  pamoja na panga zimepatikana  katika tanuri la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.

Habari zinapasha pia kwamba katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi hilo pia limemkamata mtu mmoja anayehisiwa kuwa ni  jambazi  akiwa na bomu  juu ya mti, na kwamba mtu huyo ambaye hakufahamika jina alikutwa juu ya mti majira ya jioni ya leo. 

Jeshi la polisi nchini tayari limetangaza dau  la shilingi millioni 10 kwa mtu yeyote atakaye fanikisha kuwakamata au kuwabaini waliohusika na vitendo hivyo. Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea kwa kadri zitavyopatikana

Chanzo: Michuzi Blog

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa