Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BAADHI ya Wananchi wilayani Geita mkoani hapa, wamemuomba Mkuu wa
Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu kumrudisha aliyekuwa Kamanda wa
Mkoa, Leonard Paulo aliyehamishiwa Marogoro hivi karibuni.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wakazi hao walisema, wanaomba
hivyo kutokana na kukithiri kwa mauaji yanayosababishwa na majambazi,
ambao wamefanya wakazi wa mjini hapa kukosa amani na kushindwa kufanya
kazi zao za kila siku kwa kuogopa kuvamiwa.
Mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Mashanja Juma
kutoka Katoro, alisema kipindi yupo Kamanda Paulo, majambazi waliisha
na mauaji ya vikongwe yalipungua kwa kasi, lakini kwa sasa vikongwe
wanazidi kukatwa mapanga na kuuawa huku majambazi wakizidi kumaliza
maisha ya watu.
Juma, aliongeza kuwa matukio makubwa ambayo yametokea kipindi kifupi
tangu Kamanda Paulo aondoke ni lile la kuvamiwa wafanyabishara wawili
na kuuawa mmoja wao, Gozibert Walwa aliyeuwawa majira ya saa 11 jioni.
Alisema tukio la pili ni lile la kutekwa kituo cha polisi Bukombe na kuuwa askari wawili na kuibwa silaha mbalimbali.
Chanzo; Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment