Home » » HATARI: WANANCHI WATEKETEZA KAYA NNE ZIKIWEMO ZA VIONGOZI WA KIJIJI CHATO‏

HATARI: WANANCHI WATEKETEZA KAYA NNE ZIKIWEMO ZA VIONGOZI WA KIJIJI CHATO‏

WANANCHI wenye hasira kali katika kijiji cha Beda Kinsabe kata ya Iparamasa Wilayani Chato Mkoani Geita wamebomoa nyumba za kaya nne na kuzichoma moto zikiwemo za viongozi wa serikali ya kijiji hicho na kuteketeza mali mbalmbali zikiwemo mashine za kusaga mawe ya dhahabu baada ya walinzi wa kampuni ya JOMA SECURITY LTD tawi la Katoro kudaiwa kumuawa juzi raia mmoja ambae ametambulika kwa jina moja la Emanuel (30) kwa kipigo hadi kufariki dunia ambaye alikuwa akituhumiwa na mwajili wake Shaban Ramadhani kumwiibia kifaa cha mashine ya kusaga mawe ya dhahabu (Karasha) chenye thamani ya shilingi laki sita (600,000) . Akisimulia tukio hilo Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Silas Mpanda ambaye pia ni mmoja wa athirika wa tukio hilo amesema lili tokea usiku wa kuamkia septemba 19 majira ya saa mbili usiku na kudumu hadi majira ya saa nne usiku polisi walipo fika kijiji hapo na wananchi kutimua mbio . Alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni walinzi wa kampuni ya Joma Security Ltd wanao fanya kazi ya ulinzi katika soko la kijijini hapa kumuwa raia mmoja kwa kipigo ambaye alifikishwa katika ofisi ya kitongoji cha Beda na aliyekuwa mwajili wake Shaban Ramadhani akimtuhumu kumwiibia kifaa cha mashine na kisha kumkabidhi kwa walinzi hao wa mshughulikie hadi kifaa hicho kipatikane ndipo walinzi hao walianza kumshushia kipigo na kupelekea kufariki dunia . ‘’’Wananchi wameamuwa kumalizia hasira kwa viongozi kwa kuwa sisi ndiyo tuli kubaliana kwa kushirikiana na wafanyabiashara tuka waleta walinzi kwa ajili ya ulinzi hii ni baada ya kukithili kwa matukio ya watu kuvamiwa na majambazi hapa hatuna ulinzi shirikishi watu waliopo hapa wengi wamekuja kiutafutaji alisema Mpanda Ofisa mtendaji wa kata ya Iparamasa Christopher Mabuba akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni walinzi wa kampuni ya Joma security Ltd kudaiwa kumuawa kwa kipigo mtu mmoja ambaye alitambulika kwa jina la Emanuel ambae alikuwa akituhumiwa na aliye kuwa mwajili wake Shabani kumwiibia kifaa cha mashine ya kusaga mawe ya dhahabu ndipo wananchi waka jichukilia sheria mkononi . Aliwataja walio bomelewa nyumba zao na mali zao kuteketezwa kwa moto kuwa ni pamoja na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Silas Mpanda ,Mayunga Jeremia mwenyekiti wa kitongoji cha Beda Shaban Ramadhani Adam Mazuri . Aidha alisema kuwa mali mbalimbali zikiwemo mashine za kusaga mawe ya dhahabu Jenereta Tv vyakula nguo pamoja samani za ndani vina kadiriwa kuwa na zaidi ya milioni mia mbili hamsini zimeteketea . pia alisema kuwa walinzi watano wa kampuni hiyo pamoja na Mfanyabiashara Shaban Ramadhani na Mayunga Jeremia ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji cha Beda wana shikiliwa na jeshi la polisi wilayani Chato . Pia aliongeza kuwa jeshi la polisi lili wahi kufika katika eneo la tukio na wananchi kuamuawa kutimua mbio na kwamba wange chelewa kufika kijijini maafa yange kuwa makubwa zaidi Habari za uhakika kutoka katika eneo la tukio zimeeleza kuwa marehemu Emanuel alibambikizwa tuhuma ya wizi wa kifaa hicho na mwajili wake Shabani baada ya kumdai malimbikizo ya malipo ya mshahara wake kiasi cha shilingi laki nane (800,000) kwa kazi ya kuopareti mashine za kusaga mawe ya dhahabu hali ambayo ilipelekea kutofautiana na mwajili wake na kwamba wananchi hao walipatwa hasira baada ya kubaini kuwa uongozi wa kijiji unafahamu undani wa tukio hilo lakini uliamua kufumbia macho suala hilo na kutaka marehemu azikwe kinyemela mwili wa marehemu ulikutwa katika ofisi ya walinzi wa kampuni hiyo baada ya kutoka katika ofisi ya mwenyekiti wa kitongoji cha Beda. Msemaji wa kampuni ya ulinzi Joma Security Ltd tawi la Katoro S.S. P .V Peter Eliasi akiongea na mwandishi wa habari ofisini kwake akiri walinzi wa wa tano wa kampuni hiyo kushikiliwa na polisi ambao ni Maneno Mabula , Ramadhani Ndama ,Abel Mpigachai , Mazuri Adam pamoja na Magida huku akiuutupia lawama uongozi wa serikali ya kijiji hicho kukeuka utaratibu na kuwa tumia walinzi wa kampuni kwa maslahi binafisi bila uongozi wa kampuni hiyo kufahami shwa ‘’’ unajua uongozi wa kijiji ndiyo umehusika katika hili moja kwa moja kwa kuwa tumia walinzi wa kampuni kama askari mgambo wa kijiji hilo ni kosa alisema Peter . Mwandishi wa habari alifika juzi kijijini hapo na kushuhudia magari mawili ya polisi moja kutoka katika kituo kidogo cha polisi Buseresere pamoja kutoka katika kituo cha polisi wilayani chato lenye namba za usajili PT 19999 likiwa wasaka watu wanao tuhumiwa kuhusika na tukio hilo sambamba na kuhakikisha amani ina rejea kijijini hapo na pia alishuhudia huduma za jamii kusimama baada ya maduka kufungwa huku baadhi ya wanaume wakiwa wamezikimbia familia zao wakihofu kutiwa mbaroni na polisi . Kamanda wa polisi mkoani Geita Kamishina Msaidizi Joseph Konyo akiongea kwa njia ya simu alithibitisha kuwepo kwa tukio na kwamba watu saba wanashikiliwa wakiwemo walinzi wa tano wa kampuni hiyo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa