Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SIKU chache baada ya Tanzania Daima kuandika habari iliyokuwa
ikiwatuhumu Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maweda Gwesandili na
Mtendaji wa Kata ya Isulwabutundwe, Sadik Masalu kuiba sh. milioni 1.2
za wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu wameanza kuzirudisha.
Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili, umebaini kuwa viongozi hao hadi sasa wamesharudisha sh. 800,000.
Kaimu Mtendaji wa kata hiyo kwa sasa, Joel Nguku, alisema kuwa Diwani
Maweda na mtendaji wake wameamua kurudisha pesa hizo baada ya Tanzania
Daima kuandika wizi huo na wananchi kutishia kuwaburuza mahakamani
kutokana na wanafunzi hao kukosa masomo.
Nguku, aliongeza kuwa pamoja na viongozi hao kuanza kurudisha pesa
hizo, lakini Masalu ambaye ni mtendaji amekataliwa na wananchi wa kata
hiyo kuendelea kukaa hapo.
Nguka amelipongeza gazeti la Tanzania Daima kwa kutoa taarifa hiyo
iliyosaidia watuhumiwa hao kuanza kurejeshwa kwa fedha za wanafunzi
hao.
Tanzania Daima Jumapili, lilimuuliza Diwani Maweda kuhusu kurudisha
pesa hizo ambapo alikiri kurudisha shilingi laki nne ambazo alisema
alikuwa amezikopa na nyingine zinazobaki anatakiwa arudishe mtendaji
wake ambaye alichukua nyingi zaidi.
Naye mtendaji alipoulizwa lini atarudisha pesa alizokwapua alisema
kuwa pamoja na kuzichukua pamoja na diwani, lakini anashangaa kuona
mpira unaangukia kwake.
“Mimi namshangaa diwani wangu anasema kuwa mimi nilichukua pesa
nyingi na huku tuligawana, wote tunatakiwa turudishe nusu kwa nusu,
sijui kwanini diwani anawaambia wananchi kwamba pesa zote niliiba mimi,
huo ni uongo,” alisema Masalu.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment