Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma, amelaumiwa
akidaiwa kuingilia maamuzi yanayofikiwa na Baraza la Madiwani, likiwemo
la ujenzi wa choo.
Kutokana na shutuma hizo, baadhi ya madiwani walitishia kuandika
barua ya kumtaka waziri mwenye dhamana na mamlaka za miji kuifuta
Halmashauri ya Mji wa Geita kwa kile walichodai ‘kuporwa’ uhalali wake
wa kujiamria mambo yake kwa mujibu wa katiba.
Diwani wa Bulela, Boniphas Fulano, alimshutumu mwenyekiti huyo kwa
madai kuwa amekuwa akiingilia na kuvuruga maamuzi yao. Alidai baraza
hilo liliamua kuvunja soko la Shilabela na Nyankumbu yaliyopo barabarani
kwa ajili ya usalama wa wananchi, lakini mwenyekiti huyo alienda kuzuia
agizo hilo.
Katika mgogoro wa ujenzi wa choo cha wafanyabiashara, kiongozi huyo wa CCM aliamuru kisijengwe kiasi cha kusababisha vurugu.
“Na suala la ujenzi wa choo hiki cha soko kuu baraza lilikaa Aprili
30, mwaka huu na kuamua ufanyike, na akiwa na taarifa za hatua zote,
lakini amekuwa akiwaingilia bila kufuata utaratibu wa kiuongozi, hivyo
kuonekana halmashauri hii haina maana kuwepo,” alisema Filano.
Hata hivyo, Msukuma alijitetea akidai kuwa alichukua uamuzi huo baada
ya kupata malalamiko kwa wananchi kuwa hawajashirikishwa katika ujenzi
huo, hivyo alifikia uamuzi wa kufukia mashimo ya msingi yaliyokuwa
yameanza kuchimbwa na mkandarasi aliyekuwa amepewa kazi hiyo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment