WALIMU 97 katika shule ya msingi Nyankumbu na Mkombozi
katika Wilaya ya Geita, wanatumia tundu moja la choo ambacho kipo kwenye nyumba
ya mwalimu huku wanafunzi wa shule hizo 3,563 wakitumia matundu 14 ya choo na
kuhofiwa kutokea magonjwa ya milipuko.Taarifa za awali kuhusu tatizo hilo
zinadai kuwa, baadhi ya walimu wamekuwa wakiulalamikia uongozi wa halmashauri
hiyo kwa muda wa miaka mitano hadi sasa, bila kusikilizwa licha ya uongozi wa shule
kuandika barua kwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutaka tatizo hilo
kutatuliwa.
Baadhi ya wanafunzi wakiongea na mtandao huu Juni 6, 2014
wamedai kuwa wamekuwa wakipata usumbufu wakati wa kujisomea kutokana na shule
hizo kukosa madawati yakutosha na wakati mwingine kuhofia kula vyakula
mbalimbali kutokana na hofu ya kupata magonjwa ya milipuko.
Akizungumzia tatizo hilo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi,
Nyankumbu, Jasmin Ngume, amesema awali ilikuwa shule moja na baada ya muda
uongozi wa Halmashauri hiyo, ilifanya utaratibu wa kuzigawanya na kuwepo na
shule ya msingi Mkombozi na Nyankumbu, ambazo hadi sasa zinakabiliwa na
matatizo ya miundombinu ya madarasa na vyoo.
“Tangu walivyofanya utaratibu wao tumeendelea kutumia tundu
moja kwa walimu wote lakini wanafunzi waligawana matundu Saba kwa kila shule”
alisema Ngume.
Shule zetu
Amesema kwa mujibu wa taratibu za Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi, uwiano wa vyoo kanuni zinaeleza kuwa walimu wa kiume wanne
wanatakiwa kutumia tundu moja na walimu wa kike watatu wanatakiwa kutumia tundu
moja, na wanafunzi wakiume watatu hutumia tundu moja na wakike wanne hutumia
tundu moja jambo ambalo halipo katika shule hiyo.
“Hili tatizo limekuwa kubwa kwa maana wakati mwingine
wanafunzi wamekuwa wakienda kujisaidia kwenye nyumba za majirani na wakati
mwingine wanazuiliwa, jambo ambalo linatulazimu wakati mwingine kuwarudisha
nyumbani mapema ili wakajisaidie huku muda wa kazi ukiwa bado ukiwa haujafika”
Licha ya mkoa huo kujitahidi kuboresha miundombinu ya shule zilizopo
mkoani humo na usimamizi makini, katika uandikishaji wa wanafunzi wa awali kwa
mwaka 2014 asilimia 79.4 ya wanafunzi waliandikishwa, na kwa upande wa darasa
la Saba ni asilimia 91 wakati mwenendo wa kuripoti shuleni kwa wanafunzi wa
kidato cha kwanza ni asilimia asilimia 84
0 comments:
Post a Comment