Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbogwe. Wakazi wawili wa Kijiji cha Iyogelo, Kata ya Lulembela,
wilayani Mbogwe, mkoani Geita, Mariamu Mulahi (70) na Helena Mulekwa
(42) wameuawa kwa kukatwa mapanga.
Katika tukio hilo lililitokeza juzi likihusishwa
imani za kishirikina, lilisababisha watu watatu walijeruhiwa; Mage
Bukombe (62), Monica Charles (23) na Sekelwa Mapolu (61).
Wakizungumza katika Hospitali ya Wilaya ya Bukombe, walisema chanzo cha kuuawa kwa wenzao ni imani za ushirikiana.
Monica alisema chanzo cha kujeruhiwa ni kutokana
na kifo cha mume wake, Marko Madala aliyefariki Mei Mosi baada ya kuumwa
kichwa.
“Tukiwa nyumbani baadhi ya Wananzengo (Wanajamii)
walikuja na kutuambia wamekwenda kwa waganga wa jadi na kuambiwa kuwa,
Marko hakufa ila wamemficha kwa uchawi, huku walitutaka wanawake
tumfufue vinginevyo tutakiona cha moto,” alisema Charles.
Mage akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili,
alisema akiwa na wenzake Wananzengo waliwakusanya kwenye uwanja wa
familia hiyo na kuanza kuwatuhumu kwamba ni wachawi, na kuanza kupigwa
na kusimamiwa na viongozi kuanzia ngazi ya kitongoji.
Mume wa Helena alisema Serikali inapaswa kufuatilia kwa kina mauaji hayo ambayo yanadaiwa kusababishwa na waganga wa jadi.
Naomi Kanegele (33), mtoto wa Mariam Mlahi
akizungumza kwa masikitiko kufuatia kifo cha mama yake, aliomba Serikali
kudhibiti vitendo vya Wananzengo kujichukulia sheria mkononi kwa mambo
ya imani za ushirikina.
Mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Bukombe, Dk Nzeke
Mbogo alisema alipokea majeruhi watatu na maiti mbili kutokan ana
kushambuliwa na mapanga na kwamba, hali ya majeruhi inaendelea vizuri.
Dk Mbogo alisema kutokana na ukosefu wa elimu
vijijini watu wengi wamekuwa wakiweka mbele imani za ushirikina mbele
hata kama mtu akifa kwa malaria, jambo ambalo siyo zuri.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ,Joseph Konyo
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, lilitokea Mei 2
wanaendelea na uchunguzi.
“Ni kweli tukio hili la mauji ya vikongwe
limetokea, Mei Mosi mwaka huu na vikongwe wawili wamefariki wengine
wamejeruhiwa, tunaendelea na uchunguzi ukikamilika hatua za kisheria
zitachukuliwa,” alisema Konyo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment