Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZAZI watano mkoani Geita wamekamatwa na Polisi kwa kugoma kuwapeleka watoto wao shule na kuwalazimisha kuwaoza.
Hatua hiyo inatokana na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Geita, Saisi
Magalula, la kuwataka watendaji kuwakamata wazazi na walezi wasiopeleka
watoto wao shule.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mtendaji wa Kata ya
Ihanamilo, Aaron Ngoye, alisema amewakamata na kuwapeleka wazazi hao
polisi kutokana na kukaidi agizo hilo.
Aliwataja wazazi waliokamatwa kuwa ni Daud Hassan, Ezila Razaro,
Ramadhani Juma, Mbotolo Kabanzi na Hakiyamungu Kabinza, wote wakazi wa
Kata ya Ihanamilo na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote
kujibu shitaka hilo.
Alisema ingawa kuna changamoto nyingi kama kukosana na wazazi na
walezi wakidai watoto si wa mtendaji, lakini amekuwa akiwakamata wazazi
hao.
Hata hivyo, alisema kwa sasa baadhi ya wazazi wana uelewa kidogo wa kuwasomesha watoto wao.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment