Home » » TANAZANIA DAIMA YAPONGEZWA GEITA

TANAZANIA DAIMA YAPONGEZWA GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WASOMAJI wa gazeti la Tanzania Daima mkoani hapa wameupongeza uongozi wa Free Media Ltd kwa kuliwezesha gazeti hili kufika kwa wakati tofauti na awali.
Akizungumza na gazeti hili, mkazi wa Mkoa huo, David Mbakile , alisema kuwa awali alikuwa akilipata jioni lakini hivi sasa mambo yamebadilika wanalipata kuanzia saa 12 alfajiri.
“Zamani nilikuwa nikimsubiri kijana wangu atoke shule saa 11 jioni ndipo nimtume gazeti hili, lakini hivi sasa mambo yamebadilika, ninakunywa chai asubuhi nikiwa na gazeti langu mkononi,” alisema Mbakile.
Kwa upande wake, muuza magazeti maarufu wa mjini hapa, Paul Sabuni, alisema mabadiliko yaliyofanywa sasa na uongozi wa Free Media Ltd yamemfanya apate nakala nyingi zaidi tofauti na ilivyokuwa awali.
Alisema hatua la kuliwahisha gazeti hilo imewawezesha wapenzi na wasomaji wake kupata taarifa kwa muda muafaka.
“Kutokana na hali hiyo, gazeti hilo limeanza kutafutwa asubuhi na mapema kwenye vibanda vya wauzaji, tofauti na ilivyokuwa awali walikuwa wakisubiri hadi jioni, wakati mwingine kesho yake,” alisema muuza magazeti huyo.
Pamoja na pongezi hizo, wameomba uongozi wa Free Media Ltd kuzipa kipaumbele habari za mkoa huo mpya, ambao una habari nyingi, hususan za kifisadi kwa baadhi ya viongozi.
Chanzo:Tanznia Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa