Home » » WANAOUA VIKONGWE,WAHALIFU GEITA WAOMBWA KUMRUDIA MUNGU

WANAOUA VIKONGWE,WAHALIFU GEITA WAOMBWA KUMRUDIA MUNGU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WANAOJICHUKULIA sheria mkononi kwa kuwaua wahalifu na vikongwe kwa imani za kishirikina mkoani hapa, wametakiwa kuacha tabia hiyo kwa sababu wanaenda kinyume na neno la Mungu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemble of God (TAG) Jimbo la Geita, Simon Masunga, kwenye mkutano wa siku nane unaoendelea katika Viwanja vya Kalangalala vilivyoko mjini hapa.
Askofu Masunga alisema baadhi ya wakazi wa Geita huwa wanajichukulia sheria mkononi kwa kuwaua vikongwe na wahalifu kwa kuwachoma moto kutokana na kutomjua Mungu.
Alisema wakazi hao wamejikita kwenye mambo mengi ya kidunia kuliko kumuweka Mungu mbele, lakini alisema yeye na waumini wanajitahidi kuwaombea wenye tabia hiyo waokolewe na kuacha dhambi hiyo.
Pia Askofu Masunga aliwakemea wachungaji wanaofungua makanisa kwa ajili ya uchochezi au kukashifu dini nyingine kwa kuwaambia waache tabia hiyo na badala yake wafanye kazi ya Mungu.
 Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa