Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMPUNI ya Geita Gold Mine (GGM) inatuhumiwa kumpora mzawa, Hosea
Katampa, eneo lake lililopo Lijeti namba tatu licha ya kwenda
mahakamani kulidai na kupewa kihalali.
Katampa alitoa malalamiko hayo juzi alipozungumza na waandishi wa
habari waliofika eneo hilo na kumuomba Waziri wa Nishati na Madini,
kuingilia kati mgogoro huo ili arudushiwe eneo lake.
Alisema mgodi huo ulianza kulichimba eneo lake aliloanza kulimiliki mwaka 1988 bila kuwapo kwa makubaliano yoyote.
Ofisa Mahusiano wa mgodi wa GGM, Joseph Mangilima, alipoulizwa
alisema: “Namfahamu Katampa na kesi yake naijua alishinda kihalali
mahakamani sasa suala la kwa nini hajarudishiwa eneo lake mimi
nashindwa kuelewa”.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment