Home » » Wabambwa na sare za JWTZ

Wabambwa na sare za JWTZ

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

WAKAZI wa mtaa wa Ihayabuyaga, mjini Geita, wamekamatwa na polisi wakiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na pingu. Waliokamatwa ni Zakayo Odengo (21) na Mussa Emanuel (20). Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paul, alisema askari waliokuwa doria saa mbili usiku katika eneo hilo waliwatilia shaka watu hao, ambao baada ya upekuzi kufanyika nyumbani kwao walikutwa na sare hizo. Alisema ndani ya begi jeusi walikuwa wametunza pea moja ya sare za JWTZ, pingu, kofia, sare za skauti na zingine za kampuni binafsi ya ulinzi. Kamanda alisema sare hizo inasadikiwa zilikuwa zikitumika katika matukio ya uhalifu. Paul alisema watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani. Aliwaomba wananchi kutoa taarifa kuhusu watu wanaowatilia shaka. Pia aliagiza wananchi wanaomiliki sare za majeshi na silaha kinyume cha sheria wazisalimishe kituo chochote cha polisi.
Chanzo;uhuru Online

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa