Rais Jakaya Kikwete
Badala yake, Rais Kiktwete amewataka watendaji hao kuwaelimisha wakulima faida ya matumizi yake.
Alitoa agizo hilo kwa uongozi wa Mkoa wa Geita mwishoni mwa wiki baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo katika Ikulu ndogo.
Aliyasema hayo baada ya kuelezwa kuwa wakulima mkoani Geita wameridhia kutumia mbegu za pamba zisizokuwa na manyoya.
''Kumekuwapo na madai ya baadhi ya wakulima hapa nchini wanaohoji au kupinga matumizi ya mbegu mpya za pamba zisizo na manyoya kukamatwa na kufikishwa mahakamani. Hii ni kuwafanya waichukie serikali yao.
Waelimisheni waamue wenyewe badala ya kutumia nguvu," alisema Rais Kikwete.
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula, alisema hakuna tukio kama hilo la wakulima kukamatwa na kufikishwa mahakamani mkoani kwake.
Magalula alisema badala yake elimu imetumika kuwaelimisha wakulima. "Wakulima wamekuwa wakielimishwa kwa kupanda mbegu zisizo na manyoya, mavuno yake ni kilo 800 kwa ekari moja wakati mbegu zenye manyoya ni kilo 300 kwa ekari, hivyo kubainisha faida yake na kuwaacha waamue wenyewe," alisema.
Hali ya kilimo cha pamba kimekuwa kinasuasua katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ukiwamo Mkoa wa Geita kwa takribani miaka 10 sasa kutokana na kuporomoka kwa bei ya pamba kwenye soko la dunia.
Aidha, wakulima wanashindwa kumudu gharama za pembejeo licha ya kuwapo utaratibu wa ruzuku.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment