Jeshi la Polisi mkoani
Geita,limefanikiwa kuwakamata watu wawili wakiwa na kadi 243 za watu mbalimbali
wilayani Chato, zinazotumika kutolea fedha kwenye ATM za Benki ya NMB kinyume
cha sheria.
Kamanda wa polisi
mkoani Geita, Leonard Paulo,aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake,kuwa
tukio hilo lilitokea juzi saa 7, usiku katika Kijiji cha Kitela wilayani Chato.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwani
Gidion Matiku (22) na Seleman Hassan(30) mkazi wa Chato wote wakiwa
wafanyabiashara wa duka la nafaka pamoja na vifaa vya ujenzi.
“Tunawashikilia watu hawa tukiendelea
kufanya uchunguzi zaidi kwa nini wanamiliki hizi kadi zote za ATM zilizotolewa
na Benki ya NMB wanazifanyia nini kwa sababu zina majina ya wateja mbalimbali,
ambao ndio wamiliki halali wanaotambuliwa na benki hii na si wao,” alisema
Kamanda huyo.
Alisema, kuwa kitendo hicho cha
kumiliki kadi hizo za benki,ni kinyume cha sheria na kuwa jeshi hilo bado
linaendelea na uchunguzi zaidi ambapo pindi ukikamilika watuhumiwa hao
watafikishwa mahakamani mara moja.
Katika hatua nyingine,jeshi hilo
linawashikilia watu wawili wakazi wa kijiji cha Runzewe wilayani
Chato,wakituhumiwa kutaka kumuua kwa kumkata mapanga mkazi mmoja wa kijiji
hicho kwa kinachodhaniwa ni ugomvi wa shamba.
Kamanda wa polisi mkoani Geita,Leonard Paulo,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Bw.Marco Mathias (46) na Bw.Boniphace Shija (33) wote wakazi wa kijiji hicho na
kuwa tukio hilo lilitokea juzi.
Chanzo: Majira
0 comments:
Post a Comment