Home » » HOT NUUUZ: WATOTO WA KIKE GEITA WATOA TAMKO KUPINGA KUNYANYASWA KIJINSIA‏

HOT NUUUZ: WATOTO WA KIKE GEITA WATOA TAMKO KUPINGA KUNYANYASWA KIJINSIA‏



Picha ya Leah Clement aliyekatwa mkono wa kushoto hivi karibuni na mumewe Mussa Mtobeka anayeshikiliwa na polisi kwasasa hivi  akiwa hospitali ya wilaya ya Geita


Na Denice Stephano Geita yetu Blog

WATOTO wa kike kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari mkoani Geita wametoa tamko lao kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa kama watoto wa kike.

Tamko la watoto hao lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike ilyoadhimishwa Kimkoa katika Kata ya Nkome iliyo katika Wilaya ya Geita na kuhudhuriwa na watoto shule mbalimbali za  msingi na sekondari za mkoa wa Geita.

Katika tamko lao watoto hao wameitaka jamii kuacha kuwadhalilisha kwa namna yoyote ili wakisema wao ni watoto kama walivyo watoto wenzao wa kiume.

Walisema mtoto wa kiume anaonekana siyo wa muhimu katika jamii kitu kinachorudisha maendeleo ya mtoto wa kike na kumkosesha thamani kwa madai kwamba hawezi kuwa wa faida katika familia na jamii .

Waliongeza kwa kusema kuwa wamekuwa wakiingizwa katika biashara za ngono ,kubakwa na baba zao wa kambo, kutoshirikishwa katika maamuzi ya kifamilia na kufukuzwa shule wakipata mimba huku mtoto wa kiume aliyefanya hivyo yeye akiachwa aendelee na masomo.

Ni kutokana na hayo watoto hao wameiomba serikali kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha haki za mtoto wa kike  zinalindwa ikiwemo ya kupatiwa elimu stahiki.

Aidha wametaka ubaguzi wa kijinsia usiwepo pia waliiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya kijinsia kwa jamii na kuwachukulia hatua kali sana wote wanaokatisha masomo watoto wa kike kwa namna yoyote ile.

Awali kabla ya tamko la watoto hao Meneja miradi wa shirika lisilokuwa la serikali la Plan International Serapia Minja ambao ndio waliratibu sherehe hizo aliiomba jamii kumthamini mtoto wa kike na kumwezesha kufikia ndoto za mafanikio yake.


Akijibu tamko la watoto hao mgeni rasmi Sara Mangoe aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Geita Omary Mangochie alisema serikali haitakaa kimya kwa yeyete atakayemdhalilisha mtoto wa kike .

Alisema serikali inamthamini sana mtoto wa kike hivyo itaendelea kutoa elimu kjamii ili iendelee kutambua haki za mototo wa kike na kuzulinda.

                                   NA GEITA YETU BLOG

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa