Home » » News Alert: Gari la kubebea wagonjwa lakamatwa likitumika katika wizi ndani ya Mgodi wa Geita

News Alert: Gari la kubebea wagonjwa lakamatwa likitumika katika wizi ndani ya Mgodi wa Geita

Gari la kubebea wagonjwa(ambulance) T671 AKW lililotolewa kama msaada na Mwenyekiti wa ccm Mkoani Geita Bwana MUSUKUMA kwa ajili ya kituo cha afya cha Nzera, limekamatwa na askari wa mgodi wa Geita Gold Mine, ndani ya mgodi huo eneo la kituo kikuu cha umeme mgodini humo(Geita Power) likipakia vitu mbalimbali yakiwemo mapipa yenye oil na diesel ambavyo ni mali ya mgodi kwa lengo la kuvipeleka mahali ambapo mpaka sasa hapajajulikana.

Tukio limetokea mida ya saa tisa usiku wa kuamukia leo.Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio wakiongozwa na OCD wa Geita bwana MAKONA na kuwakuta watuhumiwa wanne akiwemo dereva wa gari hilo wakiwa chini ya ulinzi wa askari wa mgodi huku mtuhumiwa mmoja akidaiwa kutoroka.

Watuhumiwa wote wapo kituo cha poloisi Geita kwa mahojiano zaidi, nafuatilia picha na majina ya watuhumiwa wote niweke hapa jamvini. 

Source: GGM SECURITY STAFF.

1 comments:

Mahangaiko said...

Da serikari tazameni hilo na msilifumbie macho kwanza amedhalilisha serikari pili kwanini aibiwe GGM kamata walo husika wote wawajibike

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa