na Ali Lityawi, Geita
WAHAMIAJI
haramu 19 kutoka nchini Burundi na raia mmoja wa Kenya wamekamatwa na Idara ya
Uhamiaji mkoani Geita wakiwa wamejificha vijijini wakifanya shughuli za kilimo
cha bustani ya mananasi.
Kaimu
Mkuu wa Uhamiaji mkoani Geita, Charles Mwandima, alisema janakuwa wahamiaji hao
walikamatwa kwenye vijiji vya Nyamilyango, Sungusila na Kakubiro.
Alisema
wahamiaji hao walikamatwa kwenye oporesheni maalumu na kwamba idadi hiyo
inaweza kuongezeka kutokana na msako huo kuendelea.
Aliwataja
wahamiaji hao waliokamatwa kuwa ni Rongino Barabonerana (38), Braiton Kiporoka
(26), Leonard Petro (25), Heshimana Marko (25), Manilambona Deo (15), Kwizela
Jacob (15), Charles Yona (24), Furaha Jovalini(23), Mateso Yusuph (17), Japhet
Philipo (19).
Wengine
ni Nyizingano Felaste (22), Bizimana Gerrald (19), Athumani John (19), Ndingwao
Gerald (17), Mawazo Samweli (21), Nimbona Miraji (19), Hatizimana Nestory (19),
Japhet Gervas (21), Jerald Mahangaiko (21) na Kevin Odongo ambaye ni raia wa
Kenya.
Alisema
watu hao walijipenyeza na kupokewa na wenyeji kinyume cha kisheria ya nchi na
wamekuwa wakiwatumia katika kufanikisha vibarua katika kilimo cha bustani ya
mananasi na watafikishwa mahakamani wakati wowote.
CHANZO MTANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment