Home » » MWENYEKITI MINKOTO AFUNGWA MIAKA MITANO JELA

MWENYEKITI MINKOTO AFUNGWA MIAKA MITANO JELA

na Lucy Ngowi
MAHAKAMA ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita, imemhukumu kifungo cha miaka mitano jela, mwenyekiti wa kijiji cha Minkoto, Alphonce Kanungu (44), na wenzake wawili baada ya kupatikana na hatia ya kuhamasisha vurugu, kuchoma nyumba na kuwakatakata ng’ombe 30 na mbuzi 20 kinyume cha sheria.
Wengine waliohukumiwa kifungo kama hicho ni Marco Elias (36) na Cosmas Kanungu (30) wote wakazi wa kijiji cha Minkoto, kata ya Bwanga.
Habari kutoka Chato zinaeleza kuwa mbali na kifungo hicho, washtakiwa hao wametakiwa kulipa fidia ya sh milioni 38 kwa mlalamikaji, Paul Mhunda.
Akitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Hakimu Khasan Koja alisema ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi, Mkwasi Rashid.
Washtakiwa hao walidai kuwa April 3, mwaka huu, majira ya saa 2 usiku waliongoza kundi la wananchi, kwenda kufanya uharibifu mkubwa wa nyumba, mifugo na mali ya Paul Mhunda na kusababisha hasara ya sh milioni 38.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa