Na Victor Bariety, Geita
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mbio za Mwenge wa Uhuru ziliingia dosari mara mbili wilayani Geita, baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Manzie Mangochie kuupoteza msafara na risala iliyokuwa imeandaliwa.
Kitendo hicho, kilichosababisha kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa, Kapteni Honest Mwanossa, kushindwa kuzindua miradi ya maendeleo.
Tukio hilo la aina yake, lililotokea juzi saa 10 jioni lilisababisha msafara huo kusimama kwa muda wa dakika 10 katika kijiji cha Ngula, kitendo ambacho kilionekana wazi kumkera Kapteni Mwanossa na kutoa karipio kali kwa mkuu huyo wa wilaya.

Msafara huo, ulishindwa kuzindua mradi wa kikundi cha kuweka na kukopa cha Nyamalimbe, ambacho kilitarajia kukaguliwa na kiongozi wa mbio hizo, kabla ya kuondoka saa 11 kwenda kukagua shamba la mihogo katika Kijiji cha Ngula.
Kapteni Mwanossa, aliamua kuusimamisha msafara huo baada ya kupita kundi kubwa la wananchi waliokuwa wamejiandaa kuupokea Mwenge wa Uhuru, wakiwa wamejipanga pembeni mwa barabara.
“Kilichoniumiza mimi ni ule wingi wa wananchi waliokuwa wamefurika pale wakitusubiri, nilidhani kuna sehemu tunakwenda kisha tunarudi kwa wale wananchi, kumbe tumewaacha? Unajua huu ndio mwanzo wa wananchi kuichukia Serikali,’’ alisema kiongozi huyo.
Katika dosari ya pili, mkuu wa wilaya hiyo, alijikuta akimkabidhi Katibu Tawala Wilaya ya Geita, Moses Minga risala ya utii ya wilaya kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, risala ya wilaya ya Nyag’hwale, badala ya Wilaya ya Geita.
Wakati akisoma risala, Minga alijikuta akisimama kwa muda kusoma risala hiyo, baada ya kubaini kuwa aliyokuwa akiisoma ilikuwa taarifa ya wilaya jirani na si Geita, ambapo alilazimika kueleza bayana kwamba taarifa hiyo ilikuwa ya Nyang’hwale, wakati huo Mwenge ukipewa heshima zote.
"Mkuu wa wilaya, hii taarifa ni ya Nyag’hwale sio ya Geita…iko wapi yenyewe ?’’ alihoji Minga, hatua iliyopelekea mkuu wa wilaya kupaza sauti mbele ya umati wa wananchi waliofurika kushuhudia tukio hilo na kumwita dereva wake kupeleka taarifa Geita.
"Peter yuko wapi?!....Peter lete risala imo kwenye gari’’ alisikika Mangochie akipaza sauti, kitendo ambacho kilidumu dakika kadhaa.
Akihutubia wananchi wa Geita, Kapteni Mwanosya aliwataka watendaji wa Serikali kusimamia matumizi ya fedha za Serikali, zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment