Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mheshimiwa
Herman Kapufi Mkuu wa Wilaya ya Geita akitoa maelekezo kwa viongozi wa
Halmashauri ya Geita na kata ya kakubilo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa
wa Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Halmashauri hiyo kuhamasisha
ujenzi wa Zahanati na vyumba vya madarasa.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa
Mkoa wa Geita akishirikiana na wananchi wa Kata ya Ludete Wilayani
Geita kumwaga zege kwa ajili ya lenta kwenye ujenzi wa madarasa 10 ya
shule ya msingi Ludete yenye wanafunzi 6,616 alipokwenda kuzindua
kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mhandisi Robert Gabriel akishirikiana na mafundi kupandisha ndoo yenye
zege kwa ajili ya uwagaji wa leta katika majengo 10 ya vyumba vya
madarasa shule ya Msingi Ludete Wilayani Geita.
Mhandisi
Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita akikabidhi fedha shilingi 2,400,000/=
kwa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Mranda kwa ajili ya ujenzi wa
boma la Zahanati ya Kijiji na Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari katika
hiyo.
Wananchi
wa kijiji cha Ludete Kata ya Ludete Wilayani Geita wakishiriki katika
uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika kijiji hicho
kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mkuu wa mkoa wa Geita za kila
kijiji kuwa na Zahanati.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akifuatilia kwa karibu
maendeleo ya wanafunzi wa kidato cha Tatu shule ya Sekondari Kakubilo
Halmashauri ya Geita baada ya kutembelea shule hiyo na kutoa swali la
Hisabati kwa wanafunzi hao.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za
ujenzi wa Zahanati na Shule kata za Ludete na Kakubilo Halmashauri ya
Geita kwa kuchangia matofali yenye thamani ya shilingi 2,400,000/= na
kufanikisha harambee ya mifuko ya Saruji zaidi ya 420.
Mhandisi
Robert Gabriel ameunga mkono jitihada za wananchi baada ya kutembelea
kata hizo na kuridhishwa na kazi za ujenzi wa Zahanati za vijiji na
Shule zinazofanywa na wananchi kwa kujitolea kufanya kazi bila malipo,
kuchangia vifaa mbalimbali vya ujenzi na kuchimba misingi.
Akiwa
Kata ya Ludete Mkuu wa Mkoa amesema " Nimefurahi sana kuona namna
mnavyoshiriki katika utekelezaji wa miradi hii niwaombe mshiriki kuanzia
mwanzo hadi mwisho na msikubali mtu yeyote kuwavunja moyo kwa kuwa
maendeleo ya Ludete yataletwa na wananchi wenyewe hivyo mimi
ninawachangia matofali 1000 kwa ajili ya Zahanati na mengine 1000 ya
kujenga vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Ludete".
Awali
akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Diwani wa Kata ya Ludete Sebastian Benedicto
Mranda amesema kuwa wananchi wameamua kujitolea kushiriki ujenzi wa
Shule mpya ya msingi baada ya shule ya Msingi Ludete kuwa na Idadi ya
wanafunzi 6,616 huku kukiwa na madarasa 20 yenye mikondo 108 ambao
unasababisha msongamano wa wanafunzi darasani.
Marando ameongeza kusema kuwa Kata ya Ludete haina Zahanati kwa muda mrefu hivyo wananchi wamejihamasisha kujenga ili wapate huduma katika maeneo yaliyo jirani pia kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati na shule ya msingi na Sekondari kwa Kata, Kata ya ludete ina wanafunzi 900 wanaotarajia kujiunga na elimu ya Sekondari ikiwa na uhaba wa zaidi ya vyumba vya madarasa 20.
Marando ameongeza kusema kuwa Kata ya Ludete haina Zahanati kwa muda mrefu hivyo wananchi wamejihamasisha kujenga ili wapate huduma katika maeneo yaliyo jirani pia kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na Zahanati na shule ya msingi na Sekondari kwa Kata, Kata ya ludete ina wanafunzi 900 wanaotarajia kujiunga na elimu ya Sekondari ikiwa na uhaba wa zaidi ya vyumba vya madarasa 20.
Katika
ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa amefanya harambee ambayo imefanikisha
upatikanaji wa mifuko ya Saruji zaidi ya 420 na kuziagiza Halmashauri
kutumia vikundi vya mafundi waliokatika maeneo ya miradi ili kupunguza
gharama na kusimamia matumizi ya fedha za miradi hiyo.
Kutokana
na Mkoa wa Geita kuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na Zahanati
Serikali imeamua kushirikiana na wananchi kufanya kampeni ya mkoa mzima
kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki na kuchangia ujenzi wa miradi
ya maendeleo ili wananchi wapate huduma katika majengo bora na mazingira
salama.
0 comments:
Post a Comment