Home » » MKAPA KUKABIDHI NYUMBA 10 HOSPITALI YA WILAYA YA CHATO

MKAPA KUKABIDHI NYUMBA 10 HOSPITALI YA WILAYA YA CHATO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Chato
RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa amewasili wilayani hapa mkoani Geita ambapo leo anatarajiwa kukabidhi nyumba kumi kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato zilizojengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.
Mkapa ambaye alikuwa ameambatana na mkewe, Mama Anna Mkapa walipokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli aliyekuwa sambamba na mkewe, Mama Janeth Magufuli.
Katika msafara huo pia Rais mstaafu Mkapa ameambatana na Balozi wa Japan hapa nchini, Masaharn Yoshida ambaye leo anakabidhi mashine ya kukamulia mafuta ya alizeti kwa chama cha Ushirika wa Kilimo na Masoko Chato (AMCOSS). Rais mstaafu, Mkapa anatarajiwa pia leo kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na mwenyeji wake Rais Magufuli utakaofanyika katika Uwanja wa Mazaina ulioko mjini
CHANZO HABARI LEO

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa