WATU 14 akiwemo Mchina, wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa katika
mgodi wa dhahabu wa Kampuni ya RZ Union Mining Ltd uliopo Kata ya
Nyarugusu mkoani Geita.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Ezekiel
Kyunga alisema watu hao wamefukiwa chini ya mgodi baada ya mlango wa
kuingilia kwenye shimo la mgodi kumeguka udongo na kujiziba.
“Usiku wa kuamkia leo (jana) saa tisa kwenye mgodi huo unaoendeshwa
na Wachina, mlango wa kuingilia mgodini mmoja ulimeguka na kujifunga
watu 14 wakiwa ndani,” alisema Kyunga.
Kyunga alisema kwa mujibu wa kitabu cha orodha ya watu wanaojiandikisha kuingia mgodini, kuna majina ya Watanzania 12 na Mchina.
Aidha, alisema mbali na watu hao 13, pia kuna Mtanzania mmoja ambaye
aliingia bila kujiandikisha na hiyo ni kwa mujibu wa watu walioshuhudia
tukio hilo hivyo kufanya idadi ya watu waliofukiwa kuwa 14. Kyunga
alisema tangu jana asubuhi jitihada mbalimbali za kuondoa udongo
kuwaokoa watu hao zinaendelea wakitumia mitambo na wataalamu.
“Kwa kusaidiana na Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM) na wataalamu
wengine, jitihada zinaendelea ili kuhakikisha tunawaokoa watu hao,”
alisema Kyunga. Alisema wakati huo huo wamefanikiwa kutoboa eneo jingine
na kupitisha mabomba ya hewa ya oksijeni ili kuwafanya watu hao
wasikose hewa.
Chanzo Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment