Mkuu
wa wilaya ya Kahama bw. Fadhili nkulu amewaongoza mamia ya wakazi wa
wilaya ya Kahama na viunga vyake katika mazishi ya watu saba waliofariki
katika ajali ya gari tarehe 24 mwezi huu katika eneo la Kanegere
wilayani Mbogwe mkoani Geita akiwemo Padri wa kanisa katoliki la
Mt.Karoli Lwanga mjini Kahama muda mfupi kabla ya mkesha wa sikukuu ya
Krismasi kuanza.
Akizungumza
katika ibada hiyo iliyoongozwa na askofu Flavian Kasala wa jimbo kuu
Katoliki Geita na hudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, dini,
siasa na waumini wa madhehebu tofauti ya dini mkuu wa wilaya ya Kahama
Bw.Fadhili Nkulu amesema msiba huo umeacha pengo kubwa kwa wana Kahama
kwani wamempoteza kiongozi shupavu wa kiroho na vijana ambao walikuwa ni
tegemeo licha ya kuwa bado walikua wanafunzi huku akiwataka wasihusishe
na imani tofauti zisizostahili.
Naye
askofu Liberatus Sangu wa kanisa Katoliki jimbo la Shinyanga amewaasa
waumini wa dini zoye kukumbuka kutubu na kuishi maisha ya kumuamini
mwenyezi mungu huku Askofu Lidorvic minde wa kanisa Katoliki Parokia ya
Mt. Karoli Lwanga Kahama ambako ndiko mazishi yalikofanyika akitoa neno
la faraja kwa waombolezaji.
Nao
baadhi ya waombolezaji na wau waliohudhuria katika mazishi hayo
wameonyesha masikitiko yao na kuzungumzia msiba huo ambao umeonyesha
kuwagusa kwa namna moja au nyingine
CHANZO MICHUZI MEDIA GROUP
0 comments:
Post a Comment