Hata hivyo, alisema kuwa asingeweza kulizungumzia suala hilo kwa
undani kwa sababu alikuwa kwenye sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarani ambayo kitaifa inafanyika mkoani Geita.
Hata hivyo, habari za uhakika kutoka katika Kitongoji cha Elimu,
Kijiji cha Kaseme kilichopo wilayani Geita ambako mwinjilisti huyo
alikuwa akiishi na familia yake zinasema kuwa alichukua uamuzi wa
kumwadhibu binti yake huyo aliyehitimu darasa la saba mwaka huu, baada
ya kumkuta akizungumza na mwanamume ambaye hata hivyo hakufahamika.
Inaelezwa kuwa baada ya kumpiga, alimchukua na kwenda naye nyumbani
na kumfungia ndani huku akiendelea kumwadhibu hadi alipofikwa na umauti.
Kwa mujibu wa shuhuda ambaye hakuwa tayari kutajwa jina gazetini,
baada ya mwinjilisti huyo kubaini kuwa amemuua mwanaye, alichukua uamuzi
wa kukimbia umbali ya kilometa moja na kujitundika mtini kwa kamba
iliyomnyonga hadi kufa.
Kamanda Mponjoli, alisema kuwa uchunguzi wa Polisi na wa madaktari
unaendelea na kwamba utakapokamilika miili ya marehemu wote wawili
itakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.
Aliitaka jamii kuwa makini wakati wa kuadhibu watoto kwa kuwa si
wakati wote wanapaswa kupewa adhabu kali na hatarishi kama vipigo
vinavyoweza kuwasababishia umauti.
Wakati huohuo, baadhi ya wakazi wa Kata ya Kaseme wanaomfahamu
mwinjilisti huyo walieleza kwa nyakati tofauti kushangazwa na hatua
aliyoichukua kwa sababu hakuwa na tabia ya uhalifu wa aina yoyote wala
ukatili.
Masaga Makanika na Magesa Masai kila mmoja kwa wakati wake alisema
kuwa mwinjilisti huyo alikuwa ni muumini mzuri wa dini asiye na rekodi
mbaya ya matukio ya kiuhalifu na kwamba hatua alizochukua zimewaacha na
maswali mengi huku wakifikiri kuwa pengine ni mipango ya Mungu au
majaribu ya shetani.
CHANZO GAZETI LA HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment