Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Mwandishi Wetu
MKUU
wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie anasema Tamasha la Pasaka ni jambo
kubwa sana kwao kwa sababu linafikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa
jamii.
Mangochie
anasema ukubwa na umuhimu wa tamasha hilo ni kutajwa kwa neno la Mungu
na waimbaji sambamba na viongozi mbalimbali wa dini wanaofika katika
tamasha hilo.
Mangochie
anasema Mkoa wa Geita una matatizo mengi ambayo yalikuwa yanahitaji
kukemewa, lakini mwaka huu Mungu amesikia matakwa ya wakazi wengi wa
mikoa hiyo ambayo ilitawaliwa na matukio ya mauaji yakiwemo ya vikongwe
na walemavu wa ngozi ‘Albino’.
“Mikoa
hii ya Kanda ya ziwa iligubikwa na shetani ambaye ni mauaji ya Maalbino
na Wakongwe ambao walikuwa wakitendewa unyama ambao Mungu alikuwa
akichukizwa nao, hivyo kupitia Tamasha la Pasaka neno la Mungu
litasaidia kuondosha madhila hayo,” alisema Mangochie.
Mangochie
anasema kupitia Tamasha la Pasaka waandaaji watasaidia wakazi wa mikoa
hiyo kuachana na kusahau matukio ya kumchukiza Mungu.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema
maandalizi ya kuelekea tamasha hilo yanaendelea vilivyo kwa ajili ya
kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.
Msama
alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 kwenye ukumbi wa
Desire ulioko mkoani Geita, Machi 27 litafanyika uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza na Machi 28 litafanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini
Kahama.
Msama
alisema viingilio kwa wakubwa ni shilingi 5000 na watoto shilingi 2000
ambako alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa
wingi kufanikisha tamasha hilo.
0 comments:
Post a Comment