Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa
Geita, wameitaka serikali mkoani hapa kuwatafutia maeneo ya kuchimba
wachimbaji wadogo wadogo kuliko kuwaacha wakihangaika na kukumbatia
wachimbaji wakubwa pekee.
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani hapa, Aliphonce Mawazo, alitoa kauli
hiyo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Soko
Kuu, huku akiwatuhumu viongozi wa mkoa kwa kushirikiana na Idara ya
Madini kutowathamini wachimbaji wadogo wadogo, jambo ambalo amesema ni
hatari kwa vijana ambao hawana ajira.
Alisema ingawa wachimbaji wadogo wadogo walipewa maeneo ya kuchimba
sehemu ya lwenge, lakini maeneo hayo hayana dhahabu na wamekuwa
wakiilalamikia serikali, ili iwatafutie maeneo ambayo wataweza kupata
chochote kwa ajili ya kuendesha maisha yao.
Katibu wa chama hicho, Soud Ntanyanga, alilaani vitendo vinavyofanywa
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita kwa kuwaingilia watendaji katika
kutekeleza majukumu yao kwa kisingizio cha kwamba chama tawala lazima
kitoe maelekezo katika kutekeleza majukumu yake
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment