Home » » BREAKING NEWS: MAJAMBAZI YAUA TENA MFANYABIASHARA NA KUPORA KIASI KIKUBWA CHA PESA HUKO GEITA

BREAKING NEWS: MAJAMBAZI YAUA TENA MFANYABIASHARA NA KUPORA KIASI KIKUBWA CHA PESA HUKO GEITA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Habari za hivi zilizoufikia mtandao huu kutoka mkoani Geita ni kwamba mji wa Geita umegeuka uwanja wa mapambano kati ya majambazi wawili waliokuwa wanatumia pikipiki na askari polisi mjini Geita.

Mapambano hayo ya kurushiana risasi yametokea mara baada ya majambazi wawili kumvamia mfanyabiashara wa Mpesa aliyejulikana kwa jina la Walwa mjini kisha kumuua kwa kumpiga risasi na kumpora pesa ambazo bado hazijajulikana thamani yake.

Mwandishi wa habari kutoka mkoani Geita Valence Robert anasema majambazi hayo yamemvamia mfanyabiashara huyo majira ya saa 11 jioni na baada ya kufanya mauaji hayo yalimvamia mfanyabiashara mwingine.

Kufuatia hali hiyo askari polisi walifika katika eneo la tukio na majambazi hao kukimbia kuelekea katika kijiji cha Nyang'wale  na walipofika eneo hilo majambazi hayo yalianza kuwarushia risasi askari polisi.

Hata hivyo habari za awali zinasema kuwa  hivi punde askari polisi mkoani Geita wamefanikiwa kuyaua majambazi hayo mawili yaliyokuwa yakitumia pikipiki.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amesema atatoa taarifa kamili muda mchache ujao.

Habari kamili itakuijia hivi punde,Tafadhali endelea kutembelea mtandao huu........

Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa