Wadau wa Bodi ya Pamba mkoani Geita wamekubaliana kuwa kampuni
zilizokopesha pembejeo kwa wakulima ndizo zitakazopewa leseni ya kununua
pamba kwa kuzingatia ushiriki wa kampuni hizo katika kilimo cha
mkataba.
Azimio hilo lilikuja baada ya baadhi ya kampuni
kushindwa kukopesha wakulima dawa za kuua wadudu, licha ya kuingia
mkataba na Serikali na kukubaliana kampuni hizo kukopeshwa dawa na Bodi
ya Pamba, kisha nao wakafanye hivyo kwa wakulima lakini walikiuka
maagizo hayo.
Akizungumza jana wakati akifunga kikao cha kawaida
cha Bodi ya Pamba, Mweyekiti wa Bodi hiyo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa
Geita, Said Magalula alisema, dawa za kuua wadudu zilitolewa na bodi ya
pamba kwa mkopo kupitia kampuni ya kusambaza pembejeo, ili yakawakopeshe
wakulima badala yake walichukua dawa hizo na kwenda kuziuza katika
maduka binafsi na wauza maduka hayo kuwauzia wakulima kwa bei ya juu.
Alisema kutokana na hujuma hiyo, bodi iliafikiana
kuwauzia pamba kampuni ambazo zitatoa mikopo kwa wakulima na
zitakazoshindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
“Nitoe onyo kwa wanaopeleka viua wadudu hivyo
kwenye maduka binafsi waache huo ni wizi na hatutawauzia pamba kampuni
ambayo haikumkopesha dawa mkulima,”alisema Magalula.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment