Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Nyugwa, Wilaya ya Nyangh’wale,
mkoani Geita, wameiomba serikali ya mkoa kumchukulia hatua Ofisa Elimu
ya Sekondari wa wilaya hiyo na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Lucas
Joshua, kwa kuuza majina yao kwa watu wakati wakifanya mtihani wa
kidato cha pili.
Wanafunzi hao wanadai viongozi hao wamewalazimisha kuwapa majina ya bandia ili kuhalalisha uovu wanaoufanya.
Wakizungumza kwa wakati tofauti juzi, wanafunzi hao walisema Mwalimu
Joshua amekuwa kinara wa kuuza majina yao na kuwapa majina bandia na
kuwataka kama wanataka ya kwao yaliyopotea kuyanunua ni kati ya sh
25,000 hadi 30,000, huku wakiambiwa majina yao ya awali yanafuatwa
mkoani kwa pesa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment