Home » » MWANAMKE APIGWA HADI KUFA BAADA YA KUIBA MAHINDI MABICHI

MWANAMKE APIGWA HADI KUFA BAADA YA KUIBA MAHINDI MABICHI

MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la Sambila Mihayo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 22  ameuawa kinyama na wananchi wenye hasira kali baada ya kukamatwa akiiba mahindi mabichi shambani katika Kitongoji cha Ilolanguli kijiji cha Mbabani Wilaya ya Geita mkoani hapa.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9:00 usiku ikiwa ni siku moja tu ya watu wote duniani kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa 2014.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho,Abel Kidesheni alifika eneo la tukio hilo na kukuta tayari mwanamke huyo akiwa ameuawa na wananchi hao huku mwili wake wakitaka kuuteketeza kwa moto.

Kidesheni amesema mwanamke huyo alikutwa akikata mahindi kisha kuyapakia kwenye mfuko wa sandarusi ndipo alipokamamatwa na wananchi ambao walimshambulia kwa mawe marungu na fimbo hadi kupoteza maisha yake.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita,Leonard Paulo amethitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kwamba uchunguzi unaoendela ikiwa ni pamoja na kuwabaini wote waliohusika na tukio hilo na kwamba hakuna mtu aliyeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Tukio hilo ni pili kutokea mkoani Geita katika kipindi kisichozidi wiki moja baada ya wanaume watano kuuawa kwa kukatwa kwa mapanga kisha miili yao kutoeketezwa kwa moto baada ya kuiba rambi rambi msibani kitongoji cha Nyantorotoro A,mjini Geita.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa