Na Denice Stephano,Geita yetu Blog
KATIBU
wa CCM mkoa wa Geita Mary Maziku amewataka viongozi wa wa ngazi zote za
Chama mkoani hapa kuwatembelea wanachama na kusikiliza kero
zinazowakabili na kuhimiza umoja na mshikamano.
Katibu huyo ambaye amehamia hivi karibuni mkoani Geita aliyasema haya juzi kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya
kushtukiza katika baadhi ta matawi katika Kata ya Kalangalala
ili kujua kama watandaji wa Chama wanatimiza majukumu yao.
Akiwa
katika Tawi la Mbugani aliwaambia baadhi ya viongozi wa tawi hili
aliowakuta aliwataka viongozi wote wa Chama kuanzia za matawi hadi ngazi
ya mkoa kuhakikisha hawakai ofisini tu bila kuwatembelea wananchama kwa
lengo la kukiimarisha Chama.
Alisema
ili Chama kiwe imara kinapaswa kuwa na viongozi wanaojituma ,ambao
wanasikiliza kero za wananchi na kuzifikisha kwenye mamlaka zinazohusika
kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.
Aidha
aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanaweka mikakati ya ujenzi wa ofisi
katika matawi ambayo hayana ofisi akisisitiza kuwa uimara wa Chama ni
pamoja na kuwa na ofisi ambako wanachama na wananchi watafika kupeleka
shida zao katika kuhamasisha hilo alichangia mifuko
mitatu ya saruji katika tawi la mbugani.
Aidha
aliwataka viongozi hao kufuatilia miradi mbalimbali inayotolewa pesa
ili kujiridhisha kama inafanywa kwa ufanisi akiwataka kutoa taarifa
kwake pale watakapohisi kuchezewa pesa ya serikali.
0 comments:
Post a Comment