Kazi ya Kuchimbua Kaburi imeanza
Uchimbuaji unaendelea na hapa mifupa inaanza kuonekana
Wahusika wa kuchimba Kaburi hilo wanachukua mifupa kwa ajili ya kwenda kwenye uchunguzi
Askari polisi wakiimarisha usalama katika eneo la tukio
Askari Polisi wakiwa wanaimarisha ulinzi wakati wa zoezi la kufukua kaburi
Mabakaki ya mifupa kama yalivyokutwa ndani ya kaburi
Sehemu ya mamia ya watu waliofika kushuhudia tukio hilo
Wananchi wakiwa wamelizunguka gari la polisi wakitaka kujua kilichofukuliwa
*********
SIKU
chache baada kulipotiwa tukio la mtoto Shaban Maulid (15) anayedaiwa
kufariki miaka miwili iliyopita na kuonekana tena akiwa hai, hivi
karibuni,kaburi lake anakodaiwa kuzikwa sasa lafukuliwa kwa ajili ya
uchunguzi wa kitaalam wa DNA
Tukio
la kufukua kaburi hilo lilifanyika Jana 03.10.213
majira saa 08:30 asubuhi na kusababisha shughuli za kawaida katika mji
wa Geita na mitaa yake kusimama kwa muda kwa ajili ya wakazi wa maeneo
hayo kwenda kushuhudia tukio hilo lililostaajabisha wengi.
Ilipofika
majira ya saa moja na nusu asubuhi watu walianza kumiminika
nyumbani kwa baba wa mtoto aliyefariki kisha kuonekana na ilipofika
majira ya saa mbili maofisa wa jeshi la polisi Mkoani hapa wakiambatana
na mtaalamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu kanda ya ziwa waliwasili eneo
hilo.
Aidha
zoezi hilo lilifanyika kwa amani baada ya askari polisi waliovalia sare
na makachero kuimarisha ulinzi eneo hilo ambapo mamia ya wakazi wa
Geita mjini na wale wa maeneo ya jirani kufurika eneo hilo kushuhudia
tukio zima.
Akizungumza
mara baada ya kufukua mabaki hayo mkemia huyo kutoka ofisi ya Kanda
Lucas Ndunguru alisema wamechukua mifupa miwili mirefu kutoka kwenye
miguu yote miwili kwa ajili ya kwenda kupima ili kupata
ukweli halisi .
Mtaalamu
huyo alisema lengo ni kutaka kujua mtoto aliyepatika kama ndiye mtoto
wao halisi pamoja na kujua kilichokuwa ndani ya kaburi hilo,ambapo
alisema tayari wazazi wote wamechukuliwa vipimo vya DNA kwa ajili ya
kupate ukweli halisi huku akisema wanatarajia baada ya wiki mbili
watakuwa wamepata majibu .
"tunakwenda kuchunguza sasa,tayari wazazi wote tumeshachukua vipimo vyao na vile vya mtoto,hatua inayofuata ni kuchunguza na hii mifupa tuliyoichukua kwa ajili ya kulinganisha na baada ya hapo ukweli utapatikana" alisema Lucas
Hata
hivyo wakati wakiendelea kufukua kaburi hilo walipofika urefu wa futi
moja na nusu walikutana na chungu ambacho ndani yake kulikuwa na mifupa
ilisadikiwa kuwa ni ya kuku na kuleta mshangao mkubwa kwa watu .
Mtoto
huyo Maulidi Shaban alionekana amefariki ndani ya kisima cha maji
Tarehe 01.01.2011 baada kwenda kuchunga Mbuzi kisha kushindwa kurudi
nyumbani na baadaye kuonekana baada ya siku tatu akiwa amefia kwenye
kisima.
Septemba
30 mwaka huu.mtoto huyo alikutana ana kwa ana na mama yake mzazi Aziza
Ramadhan wakati maeneo ya maeneo ya mtaa Mwembeni akitambuliwa kwa kila
kitu na wazazi wake hata majirani na walimu wa mtoto huyo wote wakisema
ni yeye bila kutia shaka.
Mtoto
huyo aliyekuwa akisoma darasa la tano mwaka huo kwa sasa hajaweza
kuongea vizuri ambapo kwa mujibu wa daktari wa hospitali ya wilaya
Dr.Adamu Sijaona alisema mtoto huyo ataendelea kuwepo hospitalini hapo
kwa uchunguzi zaidi wa kiafya ambapo alisema anaendelea vizuri.
Ofisi
ya Polisi Mkoani Geita ambayo inafuatilia tukio hili kwa karibu hapa
imeendelea kuwaomba wananchi kuendelea kusubiri majibu ya Mkemia mkuu
ambapo wananchi hao walitaka kupata majibu siku ya Jana ya
kufukua kaburi hilo.
0 comments:
Post a Comment