Home » » SHIMISEMITA NYAGH'HWALE YAPATA VIONGOZI WAPYA

SHIMISEMITA NYAGH'HWALE YAPATA VIONGOZI WAPYA

Uchaguzi mkuu wa viongozi wa kurugenzi ya wilaya ya Nyang'hwale mkoani geita ya kusimia masuala ya michezo kwenye halmashauri hiyo imepata viongozi wake wapya.

Viongozi hao wamepatikana katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana (jumatano) kwenye kituo cha walimu Kharumwa na kuwahusisha watumishi wa idara za serikali za mitaa wilayani humo.

Kwa mujibu wa ofisa michezo wa Halmashauri ya Nyang'hwale Mery Mpemba katika uchaguzi huo uliokuwa na wapiga kura 29 ulimchagua, Narshoni Magumba kuwa mwenyekiti,makamu mwenyekiti Alone Koloneri,katibu mkuu Tibianus Peter,katibu msaidizi Veronica Ndemboulanga na nafasi ya mweka hazina alichaguliwa Peter Mkinga.
Mpemba amesema wajumbe watatu wa mkutano mkuu walichaguliwa, Simon Shija, Bakari Masatu, Zuberi Stephano.

Viongozi hao watakuwa na jukumu kubwa la kusimiamia shirikisho la michezo serikali za mitaa(shimisemita)wilayani humo kwa kuwashirikisha watumishi pamoja na kuhakikisha clabu ya kurugenzi inapata usajili halali wa kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ya michezo ndani ya mkoa na taifa kwa ujumla.





0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa