na Lucy Ngowi, Chato
MAKADA 201 wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Mwenyikiti wa Kitongoji cha Buhungu, Kata ya
Kigongo, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wamejiunga na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA).
Kujiunga
CHADEMA kwa wana CCM hao kunatokana na mikutano ya vuguvugu la mabadiliko
(M4C), inayofanywa na chama hicho cha upinzani katika maeneo
mbalimbali likiwemo Jimbo la Chato, ambalo Waziri wa Ujenzi, John Magufuli
ndiye mbunge wake.
Makada
waliotimkia CHADEMA kwa nyakati tofauti ni kutoka Kijiji cha Muganza, Kasenga,
Busaka na Igando, Kata ya Bwera ambapo walidai kuchoshwa na mwenendo wa siasa
za CCM, hali ambayo imewasababisha waendelee kuwa na maisha magumu huku
viongozi wao wakiendelea kuneemeka.
Mbali ya makada
hao wengine waliojiunga na CHADEMA ni Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM kata ya
Muganza Paulo Malulu, Katibu wa Tawi la CCM Kijiji cha Mkombozi, Christopher
Charles na Mwenyekiti wa kitongoji cha Buhungu Kata ya Kigongo, Razaro
Busumabu.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo, kwenye Kata ya Muganza, Katibu
Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Chato, Alex Mukama, alisema wananchi wa Jimbo la
Chato wamekipokea chama hicho tofauti na awali waliogopa kujitokeza hadharani.
Kwa upande wake
Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chato, Mange Ludomya, aliwataka wananchi kukipa
kisogo CCM kwa kuwa kimeshindwa kuboresha maisha ya wananchi kwa miaka yote.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment