Home » » Mtoto wa miaka miwili abakwa na mjomba wake

Mtoto wa miaka miwili abakwa na mjomba wake



Na David Azaria Geita Yetu

MTOTO mmoja (jina Limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka miwili na nusu anayeishi katika kijiji cha Buseresere kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita amejeruhiwa vibaya sehemu zake za siri baada ya kubakwa na mjomba wake.

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa moja usiku nyumbani kwao na mtoto huyo,ambapo mjomba anayedaiwa kutenda unyama huo ametajwa kwa jina la Tatizo Lubalaza (20) mkazi wa kijiji hicho.

Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka kwa mama mkubwa majeruhi huyo siku ya tukio yeye alikuwa chumbani akitandika kitanda na kumuacha mdogo wake akiwa na huyo mjomba wake amembeba.

Alisema baada ya mjomba a mtoto huyo anayesadikiwa kuwa alikuwa amelewa kufika nyumbani hapo na kuingia ndani na kumkuta mtoto huyo akiwa sebuleni akicheza na mama yake mkubwa,ambapo baada ya kumbeba aliingia chumbani kwa ajili ya kwenda kutandika kitanda kwa ajili ya kulala.

‘Huyu mtoto naishi naye hapa nyumbani kwangu kwa wiki moja sasa baada ya mama yake mzazi kwenda Bukoba kwenye Biashara,nah ii si mara ya kwanza ni mara nyingi nimekuwa nikibaki naye hapa nyumbani,lakini cha ajabu juzi nimeshangaa mdogo wangu kwa kitendo hiki alichomfanyia mtoto…..’’ alisema mama Mkubwa wa Mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Pelesi Lubalaza.

Akielezea tukio hilo Pelesi alisema baada ya kuanza kufanyiwa kitendo hicho cha kikatili mtoto huyo alianza kulia kwan uchungu,hali iliyomfanya atoke chumbani mbio kuja kumuangalia,ambapo alikutana na mtoto huyo mlangoni akilia huku akiwa ameshika sehemu zake za siri.

“Nilipomnyanyua juu nikaona anatokwa na damu sehemu zake za siri na wakati huo akawa anamtaja mjomba wake,ambaye qwakati huo tayari alikuwa ametimua mbio na sikujua alikokuwa ameelekea usiku huo,nilichofanya ni kuomba msaada kwa majirani kisha nikampeleka kituo cha polisi na badaye zahanati…….’’ Alisimulia mama mkubwa wa mtoto huyo.

Alsema hakuweza kuamini mara moja kama kaka yake angeweza kufanya kitendo hicho cha kinyama kwa mtoto wao,huku akifahamu fika kwamba umri wa mtoto huyop bado ni mdogo.

Aliongeza kuwa  baada ya kugundua mtoto huyo kafanyiwa kitendo cha kinyama alichukuwa uamuzi wa kwenda kituo kidogo cha polisi cha Buseresere kwa lengo la kutoa taarifa  na kupewa barua ya matibabu  (PF3),ambapo alipelekwa katika zahanati ya Buseresere kwa ajili ya matibabu kutokana na maumivu makali aliyokuwa ameyapata.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Buseresere Joram Nyanza alidhibitisha kumpokea mtoto huyo na kudai kuwa alikuwa amechanika sehemu zake za siri na kumpatia matibabu na mkuongeza kuwa  mbali na kudhibitisha kufanyiwa unyama huo mganga huyo alisema kuwa baada ya kufanya uchunguzi wa kina aligundua kuwa hapakuwa na dalili zozote za mbegu za kiume sehemu za siri za mtoto huto ambnapo baadaye alimruhusu arejeshwe nyumbani baada ya kumsafisha na kumpatia matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi Leonard Paul alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo,alisema kwamba bado hajapata taarifa lakini akaahidi kulifuatilia kwa ukaribu na kisha kulitolea maelezo.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa