Home » » MKURUGENZI APEWA SIKU 14 KUREJESHA FEDHA ZA WALIMU

MKURUGENZI APEWA SIKU 14 KUREJESHA FEDHA ZA WALIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

HALIMASHAURI ya Wilaya ya Geita mkoani hapa imepewa siku 14 kurudisha fedha sh milioni 350 zilizotafunwa na Halimashauri hiyo ambazo walikatwa walimu wa Mkoa huo kwa ajili ya mikopo ambayo waliisha imaliza tangu mwaka 2012.
Kauli hiyo imetolewa jana na Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Chama cha Walimu Mkoa wa Geita uliofanyika viwanja vya ofisi hiyo vilivyoko magereza mjini hapa.
Mukoba, alisema kuwa zikiisha siku 14 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita anatakiwa kurudisha pesa hizo ndani ya siku hizo na asipotekeleza suala hilo, walimu wa Mkoa mzima na viongozi wake wataandamana.
Aliongeza kuwa walimu hao walikuwa wanakatwa fedha hizo kwa ajili ya kulipia mikopo yao ambayo walichukua lakini mpaka mwaka 2013 wamekuwa wakikatwa wakati mikopo yao iliisha tangu mwaka 2012.
Jamani mimi kama kiongozi wa walimu Tanzania natoa siku kumi na nne (14), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Geita kurudisha pesa za walimu wangu mara moja, asipolipa tutaandamana,” alisema Mkoba.
Awali akisoma risala ya Chama cha Walimu Mkoa Geita, Katibu Aron Masalu, alisema kumekuwa na changamoto mbalimbali kama vile walimu kuvamiwa nyakati za usiku na kunyang’anywa mali zao na kulazimiswa kuchangia mwenge kwa nguvu na wakurugenzi wao.
Masalu, aliongeza kuwa kero nyingine ni kucheleweswa kwa fedha zao za likizo na za uhamisho, japo maandalizi yanakuwa yakifanyika mapema.
chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa