Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kushoto) akimkabidhi Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Prof Ratlan Pardede Mwongozo wa uwekezaji Mkoa wa Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kulia) akifurahia jambo na Muwakilishi Mkaazi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi Jacqurline Mahon.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (Kulia) akisalimiana na Balozi wa
Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock ofisini kwake
Jijini Dar es salaam.
Na Mathias Canal, Wazo Huru Blog
Balozi
wa Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock amemuahidi Mkuu
wa Mkoa wa simiyu Mhe Antony Mtaka kuendeleza ushirikiano na Mkoa wa
Simiyu ili kuboresha sekta ya Afya kupitia Irish Aid.
Balozi
huyo ameyasema hayo wakati wa mazungumzo ya pamoja na Mhe Mtaka ambapo
tayari kwa pamoja wamekubaliana kuanza kutekelezwa wa kusudio hilo
tarehe 6 Februari 2018 kwa kuanza na timu ya wataalamu kufika Mkoani
humo ili kuanza haraka shughuli hiyo.
Balozi
H.E Ambassador Paul Sherlock amemuahidi Mhe Mtaka kuwa tayari nchi yake
ya Ireland imekusudia kwa dhati kushirikiana vyema na Mkoa huo huku
akisisitiza kuendelea kushirikiana zaidi pia katika utekelezaji wa
miradi ya Maendeleo kwenye sekta ya Mifugo, Kilimo na Utalii.
Balozi
wa Ireland nchini Tanzania H.E Ambassador Paul Sherlock ametoa kauli
hiyo ya kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka
za kutoka kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo uwekezaji wakati
alipokutana na kufanya mazungumzo leo 2 Februari 2018 katika.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amemshukuru Balozi Sherlock kwa
ubalozi wa Ireland kukubali kuwezesha safari ya mafunzo kwa wataalamu
wawili kutoka Mkoani Simiyu kwenda nchini Ireland kuanzia Februari 12
mpaka 16 Machi 2018 kwa ajili ya kupata mafunzo ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA) hasa kwenye upande wa uhifadhi wa Data za Mkoa.
Katika
hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu Mhe Mtaka alikutana na
kufanya mazungumzo na Muwakilishi Mkaazi wa shirika la Umoja wa Mataifa
linalohusika na Idadi ya watu duniani (UNFPA) Bi Jacqurline Mahon ambapo
pamoja na mambo mengine Shirika hilo limetoa zaidi Bilioni 3 kwa ajili
ya kukarabati vituo vya afya na upasuaji ndani ya Halmashauri zote za
Mkoa wa Simiyu.
Pia
UNFPA imeahidi kutoa magari kwa Halmashauri 6 za Mkoa wa Simiyu kwa
ajili ya kuboresha huduma za afya, ambapo tayari UNFPA wameamua kujenga
ofisi yao ndogo ndani ya Mkoa wa Simiyu itakayoratibu shughuli
mbalimbali za shirika hilo kwa mikoa yote ya kanda ya ziwa.
Wakati
huo huo Mhe Mtaka amekutana na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Prof
Ratlan Pardede ambaye pamoja na mambo mengine amekubali kutembelea
Mkoa wa Simiyu mwezi Macih mwaka huu 2018 huku akiwaalika wataalamu wa
Mkoa wa Simiyu nchini Indonesia mwezi Aprili mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment