Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki kuchimba msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe.
Wananchi wakishiriki kwenye ujenzi wa msingi kwenye kituo cha afya cha Masumbwe Wilayani Mbongwe.
Mkuu
wa Wilaya ya Mbongwe ,Mathar Mkupasi akizungumza na wananchi ambao
walikuwa wamejitokeza kuunga mkono jitihada za serikali za ujenzi wa
jengo la kupasulia kwenye kituo cha afya cha Masumbwe.
Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi CCM,Wilayani Mbongwe Johari Juma akisisitiza
wanachama wa chama hicho kuwa mstari wa mbele kushiriki katika shughuli
za maendeleo.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita ,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza namna serikali
ilivyojipanga kupunguza changamoto ya huduma za afya Mkoani humo wakati
alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mbongwe.
NaJoel Maduka-Geita.
Jumla ya Sh Bilioni 3 zilizotolewa na serikali Mkoani Geita zinatarajiwa kuboresha miundombinu katika Vituo saba vya afya .
Mganga
mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt Japhet Simeo alisema lengo kuu la hizo fedha
ni kuboresha miundo mbinu kwa maana ya chumba cha upasuaji kujenga wodi
ya watoto,wakina mama ,maabara na chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba
wanatarajia kuona fedha hizo zinafanyika kuboresha mandhari ya kituo kwa
maana ya bustani na majengo ambayo yamechakaa.
Simeo
alizitaja wilaya ambazo zimepatiwa fedha hizo ni wilaya 5 ikiwemo
halmashauri ya wilaya ya Geita ambayo imepewa kiasi cha sh ,Milioni 500
kwenye kituo cha afya cha Nzera na kwamba hadi sasa wameshajenga majengo
manne ambayo yamekaribia kukamilika , Mbogwe milioni 800 ambazo
zimegawa kwenye vituo viwili vya afya, Bukombe milioni 400 kwaajili ya
kituo cha afya cha uyovu , Chato wamepatiwa fedha kwaajili ya vituo
viwili ambvyo ni Bwanga Milioni 500 na Karumwa milioni 400 na Wilaya ya
Nyang’hale milioni 400 kwaajili ya kituo cha afya cha Nyang’hale.
Juma
Mabura ni moja kati ya wananchi wa Wilaya ya Mbongwe ambapo ameelezea
kuwa kumekuwape na changamoto kubwa ya upungufu wa majengo na kwamba
kukamilika kwa baadhi ya majengo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha
huduma ya afya.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Luhumbi amesema kuwa majengo yaliyo
kwenye hatua ya renta na maboma yakikamilika watakuwa kwenye asilimia 55
kwa maana ya zahanati 262 na kwamba nyingine wameanza ujenzi .
Aidha
amesisitiza kuwa lengo la serikali ni kuondoa kero ya kimiundombinu
kwenye sekta ya afya ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora za
afya.
0 comments:
Post a Comment