Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na
Bashir Yakub.
1.ZUIO LA
MAHAKAMA NININI.
Ni amri inayotolewa
na mahakama kumzuia
mtu kutofanya jambo
fulani kwa muda. Kampuni
nayo ni mtu
ambapo yaweza kuomba
zuio au kuzuiwa. Aidha yeyote ana haki
ya kuomba amri
hii ikiwa anaona
kuna jambo fulani
linafanyika na ikiwa
litaendelea kufanyika basi
litaharibu au kupoteza
kabisa kitu fulani.
Kwahiyo zuio ni
amri inayobeba maagizo maalum
kwa mtu au
watu maalum kuwaamrisha
kutoendelea na kitu
fulani kama tulivyoona
hapo juu.
Sheria ya Mwenendo
wa Madai, Sura ya 33
na Sheria nyingine
mtambuka zimeongelea kuhusu
zuio.
2. KATIKA
MATUKIO GANI UNAWEZA
KUOMBA ZUIO.
( a ) Kwa
mfano, umeshindwa kulipa mkopo
na tayari una
taarifa kuwa benki au
taasisi yoyote ya
fedha inataka kwenda kuuza
na unahisi kuna
pahala hapaendi sawa katika
mikataba yenu. Basi unaomba
zuio ili hiyo
mali yako uliyoweka
rehani isiuzwe mpaka
hapo hilo eneo ambalo
mmeshindwa kuelewana litakapopatiwa majibu.
( b ) Kwa mfano, umemuuzia mtu
gari, pikipiki, au mashine
yoyote. Mtu huyo
hajalipa kiasi cha
pesa iliyobaki kama mlivyokubaliana. Lakini anaendelea
kutumia kifaa hicho. Unaweza kuomba
kumzuia kuendelea kutumia
mpaka atakapolipa kiasi
kilichobaki ili asiendelee
kuharibu au kuzeesha
kifaa hicho.
( c ) Kwa
mfano, we ni mpangaji
katika nyumba ya kuishi au biashara.
Mwenye nyumba,eneo anataka kukutoa
kwenye pango hilo
bila kufuata utaratibu
au kwa kukiuka baadhi ya
makubaliano kwenye mkataba
wenu. Unaweza kuomba zuio asiendelee kukutoa.
Pia
mazingira mengine yoyote
ambayo unahisi kuna
kitu, jambo linataka kuharibiwa
au kuingiliwa, kuuzwa,
kupotezwa,kufichwa kinyume na
utaratibu unaweza kuomba
zuio hilo.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment