Na Evelyn
Mkokoi, Geita
Mgodi maarufu wa kuchimba dhahabu
mjini Geita wa GGM umekumbana na adhabu ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi
wa Mazingira NEMC katika Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Geita kwa kosa la kukosa vyoo vya wafanyakazi zaidi ya mia
tatu (300) katika eneo la chini ya ardhi underground
la uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Hali hiyo imeipelekea NEMC kuutoza
mgodi huo faini ya shilingi milioni 10, zinazotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi
na nne.
Katika ziara hiyo iliyomlazimu Naibu
Waziri Mpina kuvaa vifaa maluum ili kuweza
kuingia katika eneo la chini ya ardhi lenye mwamba mkubwa wa mgodi huo, akiambatana
na baadhi ya maafisa aliongozana nao katika ziara yake, Naibu Waziri alijionea
namna ambavyo eneo lenye idadi kuwa ya wafanyakazi kukosa huduma hiyo muhimu ya choo inayowapelekea kujisaidi vichakani na
kuharibu mazingira.
Aidha Naibu Waziri Mpina Pia aliweza
kujionea uharibifu mwingine unaofanywa na mgodi huo wa utiririshwaji wa Maji ya
mvua yaliyochanganyikana na madawa hatarishi kwa mazingira na viumbe hai kwenda
kwenye makazi ya wananchi.
Kufuatia hali hiyo, Naibu waziri Mpina
alielekeza uongozi wa mgodi huo kujenga miundombinu rafiki kwa mazingira
yatakayopelekea maji hayo kwenda katika mkondo sahihi..
Akiongea kwa Niaba ya GGM makamu wa
Rais wa Mgodi huo Bw. Simon Mushy, alisema kuwa wapo kwenye
mchakato wa kujenga miundombinu kwa kushiriana na Halmashauri ya Mji wa Geita.
Kwa upande wa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Katoma Bi.
Magori James Katoka alisema kuwa vumbi
na maji ya mvua vinavyotoka kwenye mgodi huo vimekuwa ni kero na changamoto ya
muda mrefu katikma kijiji hicho.
Pamoja na malalamiko mengi ya wakazi
wa Katoma Geita kuhusu uharibifu wa mazingira unaofanywa na mgodi wa GGM, Mgodi
huo pia umefanya shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kusambza
maji safi a salama katika mji wa Geita ukishirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka ya Mkoa huo.
Ziara ya Naibu Waziri Mpina Kaika
Mkoa wa geita ni muendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira, viwanda na
migodi nchini.
0 comments:
Post a Comment