Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
(Na Raymond Mushumbusi-MAELEZO)
Serikali
kushirikiana na Benki ya Dunia imejipanga kukamilisha Miradi ya Maji
iliyopo katika maeneo tofauti nchini ili kuondoa shida ya upatikanaji wa
maji safi na salama katika Vijiji,Miji,Wilaya na Mikoa.
Akijibu swali la
Mhe.Flatei Gregory Massay Mbunge wa Mbulu Vijijini (CCM) lililouliza,
Serikali imejipangaje kumaliza miradi hii ili wananchi wapate maji hasa
wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini ,Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji
Mhe. Isack Kamwela amesema miradi ya maji mbalimbali ipo katika hatua
za utekelezaji wake ili kuikamilisha ndani ya muda uliopangwa na
kuwezesha maji safi na salama kupatikana kwa wananchi.
“
Tuna jumla ya miradi takribani 1853 na miradi 1143 tayari imekamilika
na miradi 434 ipo karibu kukamilika ili kuanza kutoa huduma ya maji safi
na salama kwa wananchi walipo karibu na mradi huo”
“
Napenda kumueleza Mhe. Mbunge kuwa miradi ya maji ya Haydom, Masienda,
Tumati, Arri na Bwawa la Dongobesh ipo katika hatua mbalimbali za
utekelezaji wake na miradi yote hiyo imemalizika kwa asilimia 45 mpaka
sasa na miradi hii ya maji niliyoitaja ikikamilika itaweza kuhudumia
wananchi kama ifuatavyo Mradi wa Maji wa Haydom utakapokamilika
utahudumia wakazi wapatao 16,737, Mradi wa Maji wa Masieda utahudumia
wakazi 3,137, Mradi wa Arri utahudumia wakazi 17,580” Alisema Mhe.
Kamwela.
Akijibu swali la nyongeza toka kwa Mhe.Flatei Gregory Massay Mbunge wa Mbulu Vijijini (CCM) lililouliza
kwanini miradi hii inachelewa kukamilika, Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwela amesema miradi hii inachelewa kukamilika
kutokana na upatikanaji wa fedha za kuwalipa wakandarasi kutopatikana
kwa wakati ila Serikali inaendelea kutafuta fedha kila zinapopatikana
ili kukamilisha miradi hiyo.
Serikali kupitia
Wizara wa Maji na Umwagiliaji imejipanga kuanzisha na kuendeleza miradi
mingi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini ili kumaliza tatizo la
upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment