Home » » Mbunge mteule wa Busanda ahidi kutatua kero za wananchi Geita

Mbunge mteule wa Busanda ahidi kutatua kero za wananchi Geita

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SAMSUNG CAMERA PICTURES
 Msimamizi  wa Uchaguzi, Ali Kidwaka akitangaza matokeo ya Ubunge jimbo la Busanda na Geita.
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Mbunge mteule wa Busanda Bi Lolesia Bukwimba akiongea na Wanahabari mara baaada ya kutangazwa mshindi.
SAMSUNG CAMERA PICTURES
Diwani Mteule wa kata ya Lwamgasa jimbo la Busanda, Joseph Kaparatus akishangilia  ushindi baada ya kutangazwa kuwa mshindi.
Na Alphonce Kabilondo, Geita
MBUNGE mteule wa jimbo la Busanda wilayani Geita (CCM), Bi. Lolesia Jeremia Bukwimba amesema kuwa atahakikisha ana shirikiana na wananchi wake kutatua kero mbalimbali zinazo wakabili wanabusanda.
Bukwimba amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari muda  mfupi baada ya  msimamizi wa uchaguzi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Geita,Ali Kidwaka kutangaza matokeo ya  uchaguzi wa  ubunge.
Amesema  kuwa  kutokana  ridhaa  hiyo ambayo wananchi  wa jimbo hilo wamempa awatumikie tena ata hakikisha anatatua kero  ya  maji, afya, umeme na miuondo mbinu ya barabara.
Awali Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Busanda Kidwaka alimtangaza Bukwimba kuwa mbunge wa jimbo hilo  baada kupata kura  63,043 sawa  na asilimia 58, Ngofumani  Batist Msafiri ACT wazalendo  kura  1,532  sawa  na asilimia 1 Alphonce   Mawazo   chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA  kura  45,019 sawa  na asilimia 41.
 Kidwaka  amesema kuwa wapiga kura walikuwa  ni 68,041 na kura halali  ni 64,850  idadi ya wapiga kura walikuwa wamejiandikisha ni  109,190 .
Katika jimbo la Geita Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya hiyo, Ali  Kidwaka  amemtangaza  Mwenyekiti  wa Chama  cha Mapinduzi CCM mkoa wa  Geita, Joseph  Kasheku  Msukuma kuwa mbunge mteule  wa  jimbo hilo baada ya kupata kura 44,313 sawa na asilimia 68%  Severine   Malugu  CUF  kura 1,786 sawa na asilimia  3  Manglima  Joseph   Agustine (CHADEMA) kura 18,909 sawa na asilimia 29
Wapiga kura walikuwa ni 68,041  kura  halali ni 64.850 na waliokuwa wamejiandikisha  kupiga kura ni 109,190 .

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Geita Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa